Watawa wahimizwa kuishi maisha kama viapo vyao vinavyowaelekeza

Written by on February 8, 2017

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la DAR ES SALAM Mwadhama POLYCARP Kardinali PENGO, amewataka WATAWA wote Wakike na Wakiume KIYAISHA maisha yao ya Wakfu kama viapo vyao vinavyowalekeza na si vinginevyo.

Kardinali PENGO ametoa wito huo mwishoni mwa Wiki katika mahubiri yake, wakati wa adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu iliyokuwa maalumu kwa ajili ya kusheherekea siku kuu ya WATAWA, ambapo misa hiyo imefanyika katika Parokia ya Mtakatifu PETER CLAVEVY MBEZI LUIS.

Amesema kuwa, lengo la WATAWA hao kuweka Nadhiri Maisha ya Wakafu si kufa njaa bali ni kujitoa sadaka kwa Mungu na watu wake, huku wakiitangaza Injili ya KRISTO kwa Watu wote, kwani wao ni TAA na NURU katika Ulimwengu wa GIZA, na GIZA hilo ndilo linalopotosha  watu mpaka kufikia hatua ya kutendeana mabaya au kuuana.

Aidha Kardinali PENGO ameongeza kuwa ili WATAWA hao waweze kuwa Taa ya ulimwengu lazima waishi kikamilifu Nadhiri ya usafi wa moyo, lasivyo hawataweza kuwaangazia Watu wa Mungu, ambapo pia amewahimiza kuhakikisha wanazitii amri za Mungu kulingana na maelekezo yake Mungu, na pia wafuate maelekezo wanayopewa na viongozi wao, huku pia wakiishi maisha ya NYEYEKEVU na UTII.

Hata hivyo amewataka kila mmoja kujiuliza ni kwa kiwango gani amefaulu, kuwa NURU ya kuangazia Mataifa na kuleta UTUKUFU kwa Watu wa Mungu ndani ya Kanisa Katoliki.


Current track
TITLE
ARTIST

CLOSE
CLOSE