“Watawa someni alama za nyakati” Askofu Shao

Written by on March 9, 2018

Wakati Kanisa la TANZANIA inaadhimisha Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji, WATAWA wote nchini, wametakiwa kusoma alama za nyakati, kuwa na moyo wa kujituma bila kujibakiza, kwa kuwa wao ndio mwanga kwa Watu walio kata tamaa ya maisha.

Askofu wa Jimbo Katoliki ZANZIBAR Mhashamu AUGUSTINO SHAO amesema hayo leo wakati akitoa mafunzo kwa washiriki wanaohudhuria Kongamano la miaka 150 ya Uinjilishaji TANZANIA, linalofanyika BAGAMOYO jimboni MOROGORO, lililoandaliwa na Shirika la Roho Makatifu.

Askofu SHAO amesema kuwa WATAWA wanapaswa kutafakari zaidi nadhiri za maisha yao, ambazo zinawaalika kufanya kazi ya Utume mahali popote, bila kutazama ugumu wa mazingira ya Utume wao, bali kwa kuiga mifano ya wamisionari waliosukumwa na nia ya kueneza dini

Amesema kuwa hali ilivyo kwa sasa WATAWA wengi wanatamani kufanya kazi mazingira ya mjini na kudai vitu vya kisasa ikiwemo Redio, simu na miundombinu ya umeme, hali ambayo inawasababisha wengi wao kusahau Nadhiri zao za kutumwa popote

Aidha Askofu SHAO amewaasa WATAWA kuona umuhimu wa kuwa na mahusiano mema na wale wanaowaongoza, huku akiwaonya kuondokana na dhana ya kuhubiri juu ya dini nyingine kwa madai kwamba dini hizo ni za uongo.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE