Wapendeni na kuwathamini Mapadre, Askofu Chengula

Written by on August 9, 2018

Wakristo Wakatoliki wametakiwa kuwapenda, kuwathamini na kuwaombea Mapadre na si kutengeneza chuki miongoni mwao.

Wito huo umetolewa leo na Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA Mhashamu EVARISTO CHENGULA katika Adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu ya Upadrisho kwa Padre XAVERY MAFWIMBO, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu PATRICE VWAWA, jimboni humo.

Askofu CHENGULA amesema kuwa, kitendo cha Waamini kutengeneza chuki kwa Mapadre hakileti matokeo mazuri kwa Watoto na familia zao, kwani chuki hizo zitaendelea hadi kwa Watoto.

Aidha amewataka Wazazi na Walezi kuishi kwa upendo na kuzingatia SALA, hasa kwa kusali Biblia vifungu kwa vifungu, huku wakitengeneza familia ya Kikristo, na hiyo itaimarisha Miito kwa Watoto wao kama Ndoa, Utawa na Upadre.

Kwa upande mwingine Askofu CHENGULA amemtaka Padre MAFWIMBO kuutumia Upadre wake vizuri atakapotumwa kufanya utume wake, na awe mtii kwa Mapadre wenzake, Askofu wake na Waamini kwa ujumla.

Amemtaka kuyazingatia yote hayo kwani ndiyo yatakayomfanya aishi na kupendwa na kila mmoja, ikiwa ni pamoja na kuwa na Upendo, Huruma na ushirikiano na waamini wake.

 

 

 

 

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE