Wanautume wa Fatima nchini Tanzania, wahimizwa kusali ili kuombea Amani Ulimwenguni.

Written by on May 16, 2018

Wanautume wa FATIMA hapa nchini, wameelezwa kuwa kupitia ujumbe wa FATIMA uliotolewa na Bikira Maria kule URENO alipowatokea Watoto wa Tatu, RUSSIA, FRANCISKO na YASINTA unawaalika kuwa wamisionari wa kweli na hasa katika kuwaombea wale wote wasiomwamini KRISTO, ili wapate kumwamini na kufuata matendo yake.

Wito huo kwa Wanautume hao wa FATIMA umetolewa na Padre EVANS MSECHU, wakati akiadhimisha sadaka ya Misa Takatifu kwenye adhimisho la siku ya Bikira Maria Mama yetu wa FATIMA iliyofanyika katika Parokia ya Msimbazi Jimbo Kuu Katoliki la DAR ES SALAAM.

Padre MSECHU ambaye ni katibu wa Ndugu wadogo wa Franciskani amesema kuwa, Mama Bikira Maria ni mmisionari wa kwanza, na kwa kuwa Wanautume wa fatima wanamwakilisha yeye hawana budi kuwa wamisionari katika maisha yao yote na mahali popote pale wanapokuwa.

Aidha ameongeza kuwa wanautume wa FATIMA wanapaswa kutambua kuwa wao ni mabalozi, na kazi kubwa ya Balozi ni kuwakilisha jamii kubwa iliyoyuma yake, na sasa watambue kuwa wanayo kazi kubwa ya kuhakikisha wanaombea amani ndani ya familia, jumuiya parokia, taifa na hata ulimwengu mzima, na si kujiombea wao wenyewe tu.

Padre MSECHU amehitimisha mahubiri yake kwa kuwataka Wanautume hao kuendelea kujikita katika kusali, kwani dunia ya leo isipokuwa na amani watambue kuwa wao Utume wa FATIMA ndio sababu kubwa kwamaana wameshindwa kusali zaidi.


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE