Wakristo wakatoliki watakiwa kuipa kipaumbele SALA

Written by on February 13, 2018

Waamini wakatoliki wametakiwa kuipa kipaumbele SALA katika maisha yao kwa kuwa ni siri nzuri ya kumpenda Mungu na itainua na kuipa nguvu miito waliyonayo ndani yao.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Makamu wa Askofu wa Jimbo Kuu la MWANZA, Padre VALENTINO KABATI katika Homilia yake wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kupewa Nadhiri za Muda kwa Watawa SABA na Nadhiri za Daima kwa Sista MARIA LULU NKWABILA OSB wote wa Shirika la Mt. BENEDICTE iliyofanyika katika Viwanja vya KAWEKAMO, Jimbo Kuu la MWANZA.

Padre KABATI amesema, kila mmoja katika maisha ana Wito, hivyo anatakiwa kuuishi wito wake kwa kufuata yanayompendeza Mungu na yote yatawezekana wakiwa watu wa SALA.

Amesema ni wakati sasa kwa kila mmoja kuitika pindi YESU amwitapo na kumvuta katika wito kwa kuwa uwepo wake katika wito unaouitikia inaonyesha ni kiasi gani unampenda YESU na ni vyema kumkabidhi kila kitu cha maisha yako.

Wakati huo huo amewaomba Watawa kuwa na moyo wa kujitoa sadaka, kujaliana na kupendana Shirikani, huku akiwataka kuiga mfano wa Mtakatifu SCHOLASTIKA ambaye maisha yake yaliongozwa na SALA iliyotokana na upendo wake kwa Mungu.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE