Waamini Wakatoliki Wabatizwa nchini wametakiwa kuishi kadiri ya MIITO walioitiwa na mwezi MUNGU.

Written by on July 12, 2016

Waamini Wakatoliki Wabatizwa nchini,wametakiwa kuishi kadiri ya MIITO walioitiwa na mwezi MUNGU na wanawapasa kuwa waangalifu na nyeyekevu.

Wito huo umetolewa na Abate PRASIDUS MTUNGUJA OSB wa Abasia ya NDANDA, Jimbo Katoliki la MTWARA wakati wa Adhimisho la misa takatifu ya kuweka nadhiri za kwanza na za daima kwa Mabruda Shirika la Mtakatifu BENEDICTO, ambapo misa hiyo imefanyika katika Kanisa la Bikira Maria Msaada wa Wakristo.

Abate MTUNGUJA amesema kuwa, kila mmoja ana wito wake alioitiwa na mwenyezi Mungu, hivyo ni lazima kuwa mnyenyekevu na mpole kwani hiyo ndio silaha kubwa, na pasipo kufuata haya ni dhahiri maisha yatakuwa magumu na machungu.

Aidha amesisitiza kuwa, katika masuala ya miito na utumishi ndani ya kanisa, kila mmoja inampsa kusema ndio, huku akikemea tabia ya baadhi ya watu wanaojiuliza pindi wanapoitwa kwa kutanguliza kuwa atapata nini badala ya kutumikia.

Hata hivyo Abate MTUNGUJA amewataka Waamini wote kuhakikisha wanakuwa na imani thabiti, hata pale wanapokumbana na changamoto ndogo ndogo katika maisha yao bali wadumu katika sala.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE