Vilio, simanzi na majonzi vyatawala kuwasili kwa mwili wa Askofu Chengula Jimboni Mbeya.

Written by on November 26, 2018

MBEYA

Vilio na Simanzi na majonzi vimetawala  kwa Mapadre, Watawa wa Kike na wakiume pamoja na Waamini wa Kanisa Katoliki Jimbo la MBEYA wakiwemo Wananchi mbalimbali wa ndani na nje ya Mkoa wa MBEYA mara baada ya kuwasili mwili wa Askofu CHENGULA (IMC) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa SONGWE.

Mwili wa Askofu CHENGULA umesindikizwa na Mwalikishi  wa Papa FRANCIS, Balozi wa Vatican nchini TANZANIA, Askofu Mkuu, MAREK  SOLCZYNSKI, Maaskofu, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya  Maaskofu Afrika Mashariki na kati (AMECEA), Padre ANTHONY MAKUNDE, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. HARRISON MWAKYEMBE, na baadhi ya Mapadre walikuwa wakihudumu na kusoma katika nchi mbalimbali.

Msafara wa kuupokea Mwili wa Askofu CHENGULA  umeongozwa na baadhi ya Maaskofu akiwemo Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania na Askofu wa Jimbo la MPANDA, Mhashamu GERVAS NYAISONGA,Sheikh Mkuu wa MBEYA MOHAMED MWANSASU, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ALBERT CHALAMILA, na Viongozi mbalimbali.

Akizungumza  katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari,Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu NYAISONGA  amesema kuwa Kanisa Katoliki limempoteza  Kiongozi muhimu na kwamba atakumbukwa  kutokana na mema mengi aliyowatendea Mapadre,Watawa wa kike na kiume,waamini wa Kanisa Katoliki na wa dini mbalimbali.

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE