UWAKA tunzeni familia ZENU, asema Askofu NZINGILWA.

Written by on March 23, 2017

Wanaume Wakatoliki hapa nchini wamehimizwa kuzitunza familia zao kama ilivyo kuwa kwa Mtakatifu YOSEPH, alivyoitunza Familia yake ya Mama Bikira Maria na Yesu.

Wito huo umetolewa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la DAR ES SALAAM Mhashamu Eusebius Nzingilwa katika homilia yake wakati akiadhimisha misa Takatifu iliyokuwa maalumu kwa ajili ya siku ya umoja wa Wanaume Wakatoliki (UWAKA).

 

Katika misa hiyo iliyoadhimishwa kituo cha Hija Pugu Askofu Nzigilwa amesema, siku zote Baba ndio mlizi wa familia, hivyo ni lazima Wanaume wote wajiepushe na matendo ya ukatili dhidi ya wake zao na watoto wao, kwani Mungu aliwaumba wawe walinzi na walezi bora wa familia na si vinginevyo.

Aidha amewataka kuhakikisha wanazilea familia zao katika maisha ya Sala na ibada, kama ambavyo Mtakatifu Yoseph alimtunza na kumlea Yesu katika maisha ya Sala na ibada.


Current track
TITLE
ARTIST

CLOSE
CLOSE