Ukame siyo mpango wa Mungu, tumejitakia’ Askofu. Amani

Written by on January 20, 2017

Askofu wa Jimbo Katoliki MOSHI, Mhashamu ISAAC AMANI amesema kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi, kama UKAME na Mlipuko wa MAGONJWA, ni matokeo ya UZEMBE wa Mwanadamu katika kuhifadhi Mazingira.

Askofu AMANI ameeleza hayo hivi karibuni, wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa wa Wakurugenzi wa Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Kurugenzi ya Uchungaji, uliofanyika katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania jijini DAR ES SALAAM, na kuhudhuriwa na wakurugenzi kutoka majimbo mbalimbali Katoliki nchini.

Amesema kwamba, utunzaji wa mazingira na Usafi ni amri ya Mungu, na Watu wote wamepewa jukumu la kuhifadhi UHAI kwa kuyatunza mazingira, hivyo wakizembea juu ya jukumu hilo, lazima waonje athari za mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Wakati huo huo Askofu AMANI ameongeza kuwa, katika kusherehekea Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji na miaka 100 ya Upadri nchini TANZANIA, ni lazima kuweka mkazo wa Kuinjilisha katika familia za KIKRISTO.

Amesema kuwa nafasi ya Familia na Jumuiya katika Uchungaji ni kubwa, na kwamba nafsi ya mtu hujengeka na kuponywa katika familia.

Hata hivyo ametoa wito kwa Waamini nchini kutumia maadhimisho ya miaka 150 ya Uinjilishaji na Miaka 100 ya Upadri, kwa kufanya HIJA katika maeneo ya kihistoria, ili hija hiyo iweze kuwaunganisha Waamini pamoja na matukio ya zamani yanayowaimarisha Kiimani.


Current track
TITLE
ARTIST

CLOSE
CLOSE