Ujumbe wa Papa Francisko wa 52 wa Siku ya Mawasiliano duniani 2018!

Written by on January 25, 2018

Ufuatao ni ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa siku ya 52 ya Upashanaji wa habari duniani 2018, alioutoa tarehe 24 Januari. Siku ya Upashanaji wa habari uadhimishwa kila mwaka katika maadhimisho ya sherehe za Kupaa Bwana Mbinguni ambapo mwaka huu itafanyika tarehe 13 Mei. Ujumbe huu unaongozwana kauli mbiu “UKweli utawawekeni huru: Habari potofu (Fake news) na uandishi wa amani” Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu, anasema, katika mpango wa Mungu, mawasiliano ya binadamu ni muhimu katika kuishi umoja. Kama Binadamu ni sura na mfano wa Mungu anauwezo wa kujieleza na kushirikishana ukweli, uzuri na wema. Ana uwezo wa kusimulia uzoefu wake binafsi katika dunia na kujenga kumbukumbu ya uelewa wa matukio. Lakini binadamu kwa kuongozwa na ukiburi wake na ubinafsi hawezi kutoa mawasiliano mema kama inavyojionesha katika matukio ya Biblia katika historia ya Kaino na Abeli, hata tukio la Mnara wa Babeli. (Mw 4,1-16; 11,1-9).
Kubadilisha ukweli ni dalili ya kawaida ya upotofu ambayo mtu hufanya binafsi na kwa kwa pamoja. Kinyume chake katika imani kwa mantiki ya Mungu, mawasiliano ni sehemu ya kuelezea uwajibikaji kwa kutafuta ukweli na ujenzi wa wema. Leo hii lakini katika dhana ya mawasiliano, daima inayojionesha wepesi na ndani ya mfumo wa kidigitali,kwani yanaonekana matukio mengi ya habari za uwongo ziitwazo fake news: ma kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anaongeza kuisema wote tunaalikwa kutafakari!
Kulingana na haja hiyo Baba Mtakatifu anapendelea kutoa ujumbe wa mada ya ukweli ambayo anasema, mara nyingi watangulizi wake kuanzia mwenye heri Paulo VI (katika ujumbe wa mwaka 1972; ilikukuwa na mada ya “Mawasiliano ya kijamii katika huduma ya ukweli”). Fake news ni jambo nyeti linalojadiliwa na kitu cha mjadala! Kwa ujumla unajikita kutazama kwa kina juu ya utoaji wa habari za upotofu katika miatandao Online au katika mitandao kijamii, na ya utamaduni asili. Kwa maelezo hayo ni kusema kuwa, ni habari za uwongo, zisizo na msingi kwa uwepo wake; zenye nia ya kutaka kudanganya hadi wasomaji na watazamajiwake. Usambazaji wa fake news unaweza kujibu lengo walilokusudia, kwa kushawishi uchaguzi wa kisiasa na kukuza mapato yao kiuchumi.
Ufanisi wa fake news unajitokeza hawali ya yote mahali ambapo wao wanaigiza kwa asili yao yaani uwezo wa kutaka kuonekana na kusifika. Na hatua ya pili, habari za uwongo ambazo zinafanana, zinavutia, kwa maana ya kupendwa na kuchukuliwa makini na walengwa. Kwa kuwa na uwezo wao wa kulaghai, hufanya marudio ambayo yanasambaa kwa haraka ndani ya maisha ya kijamii na kuwatumia wenye hisia rahisi, kuziamsha kwa haraka, kwa mfano wa kuleta wasiwasi,dharau,hasira na kuchanganyikiwa. Usambazaji wa fake news unatumia kwa ujanja mitandao ya kijamii na kwa mantiki ya kuhakikisha inafanya kazi. Kwa namna hiyo mambo msingi yaliyomo ndani ya fake news, pamoja na ukosefu wa msingi, hunapata mwonekano hadi kufikia mamlaka husika kukosa uhalifu wake.
Baba Mtakatifu anazidi kufafanua kuwa, matatizo yanayoonesha kusambaa kwa fake news yametokana na kwamba watu wengi mara nyingi wako katika mazingira ya kidigitali ya pamoja, ambayo ni rahisi kupitia mantiki nyingi na maoni tofauti. Na matokeo ya mantiki ya habari potofu, ni kwamba, badala ya kukabiliana vema na vyanzo vingine vya habari, jambo ambalo linaweza kuleta uchanya wa mjadala na kufungua mazungumzo ya ujenzi, inageuka kuwa hatari hata bila utashi wa wadau wake ambao usambaza maoni ya uwongo na ushahidi. Tishio la habari potofu ni ung’oaji wa mzizi wa mwingine na uwepo wake unakuwa kama adui, hata kuwa shetani ambaye anaweza kutoa ushahidi wa migogoro ya uwongo; ndivyo habari za uwongo zinavyjionesha uwepo wake hasa tabia ya kutojali, anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko.
2.Ni jinsi gani ya kutambua? : Baba Mtakatifu Francisko anasema, hakuna hata mmoja anaeweza kusamehemewa jukumu la kupinga uongo huo! Lakini pia anatambua kwamba, si kazi rahisi, kwa maana usambazaji wa uwongo unapitia katika mazungumzo mengi ambayo yanasambaratika kichini chini pia udanganyifu wake mara nyingi ni wenye mfumo wa kisirisiri. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anasistiza kwamba iwapo inawezekana basi kuanzishwa mafundisho ambayo yanajikita hasakuchukua hatuaya kusoma na kuchunguza mantiki hiyo ya mawasiliano. Ni mafundisho ya dhati ili kuweza kuacha tabia ya usambazaji wake; kuwa na utambuzi kwamba habari zenye uwongo na kwa maana hiyo, kuwa na wadau wa kueleza wazi wahusika. Licha ya hatua hiyo ya mafunzo ni pamoja na ile ya kuanzisha taasisi na kisheria ambazo zinajikita kwa kina katika kusitisha matukio hayo, kama vile hata taaluma ya hali ya juu ya kiteknolojia na makampuni ya mitambo ya kutafuta dhana mpya ya kuhakiki na kuwatambua wahusika wanaojificha nyuma ya milioni ya picha za kidigital.
Hata hivyo Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, uzuiaji na mtambo wa ugunduzi wa habari za uwongo, hawali ya yote unahitaji hata umakini wa kina na mang’amuzi. Ki ukweli ili kuweza kuwagundua, Baba Mtakatifu anaongeza kuna kile ambacho chaweza kuelezwa kwamba ni mantiki ya nyoka, mwenye uwezo wa kujificha mahali popote ili aweze kuuma. Inahitaji mkakati wa nyoka mjanja ambaye anatajwa katika Kitabu cha Mwanzo, yeye alikuwa wa kwanza kumdanganya binadamu ikawa ndiyo fake news ya kwanza (Mw 3,1-15), baadaye ikasababisha majanga yote ya dhambi hadi kufikia mauaji ya kwanza, Kitabu cha mwanzo sura ya 4, na hata katika idadi kubwa ya mitindo ya ubaya dhidi ya Mungu, jirani, jamii na kazi ya uumbaji.
Mkakati wa uwezo huyo aitwaye baba wa uwongo kama Injili ya Yohane ilielezavyo, ( Yh 8,44) ni mkakati wa kujibuluza,wa hatari ya ulaghai kwani anatengeneza njia katika moyo wa binadamu kwa kutumia maelezo mengi ya uwongo na kutamanisha. Hayo yanajionesha katika maelezo ya dhambi ya asili, kwani, mshawishi alimkaribia mwanamke na kujifanya kama rafiki akionesha kujali wema wake, akaanza mazungumzo utafikiri ya kweli, lakini yalikuwa ukweli nusu nusu:“Ni kweli Mungu alisema: mwaweza kula matunda ya mti wowote katika bustani, lakini matunda ya mti wa ujuzi wa wema na mabaya msile…. (Mw2,17).
Mwanamke alijibu na kuelezea nyoka, lakini kwa kutaka kumfafanulia zaidi: “Tweweza kula matunda ya mti wowote bustanini, lakini matunda yaliyoko katikati ya bustanimsiuguse ili tusije tukafa (Mw 3,2) Baba Mtakatifu anafafanua, Jibu hili la mwanamke linatolewa kama vile la kisheria na lenye ugumu: kwa maana alionesha imani kwa mshawishi na kujiachia avutiwe naye, ndiyo maana laghai akabadilisha majibu hayo, akamwambia mwanamke “hamtakufa (Mw 3,4) “kwa maana alisema hivyo kwasababu anajua kwamba mkila matunda ya mti huo mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua mema na mabaya”! Mw 3,5).
Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anasema, nyoka alikuwa amefanya kazi yake ya kumwondoa mwanamke katika amri ya Mungu iliyokuwa ya wema na kufuata ushawishi wa adui shetani kwa maana “mwanamke huyo aliona kuwa mti huo ni mzuri kwa chakula na wavutia macho”… (Mw 3,6). Baba Mtakatifu anasisitiza ,katika matukio hayo ya biblia yanaonesha wazi hali halisi na msingi katika kuthibitisha na kuonesha juu ya utoaji wa habari za uongo kwamba, hakuna maelezo ya kutofahamika; kinyume chake, kuamini uongo huzalisha matokeo mabaya. Hata upotofu wa ukweli unaoonekana kidogo unaweza kuwa na athari za hatari.
Mchezo huo kiukweli unaonekana wazi katika fake news ambazo daima zinasambaa kwa namna ya haraka na rahisi, si sababu ya dhana ya kushirikishana ambayo ni mtindo wa mitandao ya kijamii, lakini pia ni kushikilia tamaa isiyoweza kushindwa ambayo inarudi kwa urahisi na inawaka katika maisha ya binadamu. Na sababu hizo wakati mwingine ni sawa na za kiuchumi na fursa za mawasiliano ya uwongo yana mizizi yake katika kiu ya madaraka, au kutaka kuwa navyo, hanasa ambapo mwisho wake tunakuwa waathirika wa kudanganyika zaidi kuliko tukio la ubaya ambao pia unazungusha uwongo wa hapa na pale ili kuiba uhuru wa moyo.
Katika dhana hiyo kuna haja ya kufundisha ukweli kwa maana ya kung’amua na kutathimini kwa kutazama utashi ambao unajikita na kuangukia ndani mwetu na unakufanya ukose wema kwa kujiingiza ndani ya kila vishawishi. Ukweli utawapeni uhuru (Yh 8,32) : Akifafanua juu ya ukweli utawapeni uhuru Baba Mtakatifu anaendelea kusema kwamba, kuendeleza uchafuzi wa lugha za uwongo uishia kuleta giza ndani moyo wa mtu, Mwanafalsafa mmoja Dostoevskij aliandika jambo maarufu akisema: anayejidanganya na kusikiliza uwongo wake, mwisho wake atafikia kushindwa kuchanganua ukweli, uwe wa ndani na hata unao mzunguka, baadaye ataanza kutotoa thamani yake mwenyewe hata wengine. Ukosefu wa kuthamini mwenyewe tena na pia mtu yeyote, ataacha kupenda na baadaye kukosa upendo, kwa maana hujisikia hujisumbu hujitenga binafsi na kuwa na tamaa na ubaya; na kutokana na maovu yake hugeuka kama mnyama, kwa maana ya mazoeza ya uongo unaoendelea (Taz Ndugu wa Karamazov, II, 2).
Je tujilinde vipi?: Mzizi wa kuzuia virus vya uongo ni kuacha kusafishwa na ukweli. Katika upeo wa kikristo ukweli si msingi ambao unatazama juu ya mambo na kutengenisha ukweli au uwongo tu. Ukweli si kupeleka mwanga katika mambo yenye giza tu: ukweli ni kutoa hali halisi ilivyo, kama vile neno la kizamani la kigiriki lisemavyo aletheia (da a-lethès) kisichofichwa, kinapelekea kufikiria.
Ukweli unajikita katika safari ya maisha yote, kwasababu hiyo, katika Biblia ,ukweli unachua, ni msaada, ni msingi, ni imani pia ni kama mzizi wa “aman” ikiwa na maana ya Amina katika neno la kiliturujia. Ukweli ni kitu ambacho tunaweza kusimama juu yake ili tusianguke. Na uhusiano wa ukweli wa kuamini ambao unastahili kuwa na matumaini ya kutambua ukweli ni Mungu anayeishi. Ndiyo uthibitisho wa Yesu; “Mimi ni ukweli (Yh 14,6) kwa maana hiyo binadamu anazidi kugundua kwa mara nyingine tena ukweli huo wakati anafanya uzoefu wake mwenyewe katika imani na kuamini anayempenda. Ni kwanjia hiyo binadamu anakuwa huru kwa maana ukweli utawapeni uhuru (Yh 8,32)
Kujikomboa dhidi ya uwongo na kutafuta uhusiano ndiyo viungo viwili ambayo haviwezi kukosa ili maneno yetu na matendo yetu yaweze kuwa ya kweli, dhati na kuaminika. Ili kupata mang’amuzi ya ukweli ni lazima kukesha, na kusema kile ambacho ni cha ukweli na kukuza wema na kupinga kile ambacho ni kinyume, kile kinachojitenga, nikagawanya na kulazimisha.Ukweli hujitenga kwa hakika pale ambapo unataka kulazimisha jambo lisilo la kawaida la kibinafsi; ukweli hutokana na mahusiano ya bure kati ya watu, kwa kusikilizana. Aidha, mtu haachi kamwe kutafuta ukweli kwa sababu kitu cha uongo kinaweza kuingia ndani yake, hata kwa kusema mambo ya kweli. Kutokana na matunda hayo tunaweza kutofautisha ukweli kwa maneno haya : ikiwa tunashawishi msuala, husabaisha migawanyiko, wengi hujuhuzulu au husababisha kutafakari na kukua kwa mazungumzo ya kujenga kwa shughuli za faida ya wote.
4. Amani ni habari njema : Baba Mtakatifu akifafanua suala hili anasema, ubora wa kuzuia uwongo si mkakati, bali ni watu: watu ambao ni huru, kutokana na kiu, wako tayari kusikiliza na kwa njia ya jitihada za mazungumzo ya dhati ili ukweli uonekane; watu ambao, wamevutiwa na mema wanawajibika hata katika matumizi ya lugha. Iwapo njia ya kuondokana na usambazaji wa habari za uwongo ni kuwajibika kwa namna ya pekee ni kujumuisha hasa wale wahusika wa ofisi za mawasiliano, waandishi wa habari na walinzi wa habari. Hawa katika ulimwengu mamboleo si kazi tu, bali ni utume wa kweli. Wanalo jukumu, licha ya uharaka wao wa kutaka kutoa habari wa kwanza, wanapaswa kukumbuka kuwa kiini cha habari si katika uharaka wa kutoa habari kwa wasikilizaji, lakini kitovu ni watu !
Kuwasilisha ni kujifunza, kwasababu inahusiana na maisha ya watu, na kwa njia hiyo kuhifadhi vyanzo na ulinzi wa mawasiliano ndiyo ukweli na mchakato wa maendeleo ya wema ambayo yanazaa matumaini na kufungua njia za mawasiliano na amani. Baba Mtakatifu anahitimisha kwa kutoa wito wa kuhamasisha uandishi wa habari wa amani ambayo si kwa maana ya kuwa unandishi wa uzuri kwa kukataa matatizo makubwa yaliyopo ya kutotoa sauti isiyo nzuri. Kinyume chake Baba Mtakatifu anasema kuna ulazima wa uandishi wa habari za kweli bila uwongo , zenye uadui na uwongo na kushikilia matukio kutangaza yaliyo kinyume,zenye kutafuta ufanisi na matangazo kama mabomu; uandishi ambao unafanywa na watu kwa ajili ya watu ambao wanatambua kama huduma ya watu wote, hasa wale ambao wako katika ulimwengu, sehemu kubwa hawana sauti: uandishi wa habari ambao haunguzi habari lakini, wanajibidisha kutafuta sababu za kweli za migogoro, ili kukuza uelewa wa mizizi na ushindi kwa njia ya mchakato wa fadhila; uandishi ambao unajikita katika kuelekeza suluhisho tofauti dhidi ya mlolongo wa habari mbaya na unyanyasaji wa maneno.
Na kwa mwaliko wa sala ya kifransiskani Baba Mtakatifu anasema,tunaweza kelekeza ukweli binafsi kwa maneno haya: Ee Bwana unifanye niwe chombo cha amani yako, Palipo na chuki nilete mapendo, Palipo na makosa nilete msamaha, Palipo na shaka nilete imani Pasipo na matumaini nilete tumaini; Palipo na giza nilete mwanga; Palipo na huzuni nilete furaha.Ee Bwana unisaidie nitamaini sana: Kufariji kuliko kufarijiwa; Kufahamu kuliko kufahamiwa, Kupenda kuliko kupendwa;Kwa kuwa:Ni katika kutoa ndipo tunapokea,Ni katika kusamehe ndipo tunaposamehewa . Ni katika kifo ndipo tuna zaliwa katika uzima wa milele.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News!


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE