TACAIDS: Watanzania Waombwa kuchangia Mfuko wa kuwasaidia waadhirika wa Virusi vya ukimwi.

Written by on September 21, 2017

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa  wa tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini Tanzania Bwana JUMANNE ISANGO,

Na Izack Boniface

Tumeya taifa ya kudhibiti UKIMWI Nchini Imewataka watanzania wote walioko TANZANIA na nnje ya nchi kujitokeza kwa nguvu zote katika kuchangia mfuko wa kuwasaidia waadhirika wa ukimwi ili kuendeleza mipango ya kuutokomeza ugonjwa huo.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini DAR ESA SALAAM kaimu mkurugenzi mtendaji wa  wa tume hiyo bwana JUMANNE ISANGO, amesema kuwa mfukohuo uliozinduliwa hivi karibuni, unalenga kuwasaidia zaidi waadhirika wa virusi vya ukimwi kwani ugonjwa huo umeendelea kuadhiri maendeleo makubwa ya taifa.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliokuwa unalenga kuangazia mwenendo wa virusi vya ukimwi nchini BWANA ISANGO amesema kuwa miaka ya hivi karibuni muenendo wa virusi hivyo umeendelea kupungua ijapo kuwa kuna tofauti ya kimikoa na hata ndani ya kimikoa, ambapo kunabaadhiya wilaya ambazo zimekuwa na maambukizi makubwa ikiwemo maeneo ya uchimbaji wa madini.

Kuhusu wastani wa kitaifa ameongeza kuwa asilimia tano nucta tatu (5.3) ni kiwango cha maambukizi ya kitaifa kwa tadhimini iliyofanyioka mwaka mwaka 2011/2012 huku akisema kuwa tafiti hizo huwa zinafanyika kila baada ya miaka minne huku wanawake wakiongoza kwa asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.8

Hata hivyo amesema kuwa mikoa inayoongoza ni pamoja na mkoa wa NJOMBE,IRINGA PAMOJA NA MBEYA na mikoa mingine yenye maambukizi kwa kiwango cha chini ni pamoja na MANYARA, TANGA LINDI NA DODOMA ikifuatiwa na mikoa mingine ambayo haijatajwa.


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE