RATIBA YA MAZIKO YA ASKOFU CHENGULA

Written by on November 22, 2018

 

Mwili wa aliekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA Mhashamu EVARISTO CHENGULA, ambaye amefariki dunia jana, utaagwa siku ya Juma tatu Novemba 26 hapa jijini DAR ES SALAAM, kabla ya kusafirishwa kuelekea Jimboni Katoliki MBEYA kwa Maziko.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kwa Vyombo vya Habari na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki TANZANIA (TEC) Padre CHARELS KITIMA, Misa takatifu ya kumuaga Hayati Askofu CHENGULA itafanyika Saa tatu kamili asubuhi katika Kanisa la Baraza la Maaskofu KURASINI Jijini DAR ES SALAM.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mara baada ya taratibu za kuaga kukamilika, Mwili wa Hayati Askofu CHENGULA utasafirishwa kuelekea Jimbo katoliki MBEYA kwa Maziko yatayofanyika siku ya Jumanne Novemba 27 katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu ANTONY wa PADUA.

Askofu CHENGULA amefariki jana NOVEMBA 21 majira ya saa tatu asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya JAKAYA KIKWETE katika Hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI alipokuwa anapatiwa matibabu.

Askofu CHENGULA alizaliwa Januari Mosi Mwaka 1941 Kijijini MDABULO na alipata daraja Takatifu ya Upadri Oktoba 15 Mwaka 1970 na Mnamo Novemba 8 Mwaka 1996 alichaguliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA na kuwekwa Wakfu kama Askofu wa Jimboni hilo Februali Mbili Mwaka 1997, na amelitumikia Kanisa kwa Miaka 48 ya Upadri na Miaka 21 ya Uaskofu.

Uongozi wa Radio MARIA TANZANIA  unatoa pole za dhati kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC, Wana Jimbo Katoliki la MBEYA, Ndugu, Jamaa na Wakristo wote TANZANIA kwa kuondokewa na mpendwa Baba Askofu CHENGULA.

 

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE