Padre Magala achakuliwa kuwa Msimamizi wa Jimbo la Mbeya

Written by on December 8, 2018

Baraza la Ushauri la Jimbo Katoliki Mbeya limemchagua Naibu Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA, Padre FRANCIS MAGALLA kuwa msimamizi wa Jimbo hilo baada ya kufariki Askofu Evaristo CHENGULA hadi hapo atakapoteuliwa Askofu mwingine.

Padre Magalla aliteuliwa na Askofu Chengula kuwa Naibu wake tangu  alipotangazwa kuwa Askofu wa Jimbo la Mbeya baada ya kuteuliwa na Papa Yohane Paulo II kushika nafasi hiyo ya uchungaji wa Jimbo.

Akitoa shukrani mara baada ya kutangazwa kuwa msimamizi wa Jimbo, Padre ameshukuru na kuomba mchakato wa kumteua Askofu wa Jimbo hilo uweze kufanyika mapema na kwamba katika wakati wa usimamizi wake  atayaenzi yote yaliyofanywa na Askofu Chengula

Aidha Baba Mtakatifu  ametoa salamu za pole kwa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) pamoja na  Mapadre, Watawa  wa kike na kiume na Waamini wote wa Jimbo la MBEYA kufuatia kifo cha Askofu CHENGULA.

Awali wakati wa misa ya Mkesha wa maombolezo  iliyofanyika Novemba,26,2018 katika Kanisa Kuu la Kiaskofu,la Mtakatifu Anthony wa Padua Parokia ya Mbeya Mjini,Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea,Mhashamu Damian Dallu  ametoa wito kwa Waamini  kuishi  kwa kufuata  sheria na taratibu za Kanisa Katoliki kwa kufunga ndoa badala ya kuishi uchumba ndani ya nyumba  kwa ni dhambi.

“Kuishi uchumba ni kila mmoja  anaishi kwao na siyo kukaa pamoja hiyo hairuhusiwi na unakuta familia zinazoishi uchumba ndiyo hizo zinatoa  watoto kuingia katika miito mitakatifu ya upadre  na utawa,”alisema.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE