Padre Asenga:Unyonge wa Padre ni tumaini la wakosefu

Written by on September 12, 2018

Imeelezwa kuwa Unyonge wa Padre ni Tumaini la Wakosefu,hivyo kila mmoja anapaswa kiushinda vishawishi vya kuwasengenya Mapadre, ambao ni daraja la kuwapeleka watu wote wenye imani mbinguni.

Hayo yamesemwa na Padre  Asenga paroko wa parokia ya Mtakatifu Augustino salasala, wakati wa ibada ya misa takatifu ya kumshukuru mungu kwa kutimiza miaka 25 ya Upadre kwa Padre John Maendeleo, mkurugenzi wa Matangazo wa Radio maria Tanzania, iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika parokia ya Mtakatifu Thomas more mbezi Mbichi Jijini Dar es salaam

Katika homimilia yake Padre Asenga ameongeza kuwa mapadre wamekuwa msaada kwa kiasi kikubwa sana kwani wana uwezo wa kubatiza watu, na  kuungamisha mambo ambayo yanazirudisha Roho za Watu, ambazo hazina mahusiano mazuri na Mungu.

Akizungumzia sababu za kuendelea kuwafariji na kuwatia nguvu mapadre padre Asenga amefafanua kuwa Kazi ya Padre ni ya kutakatifuza watu na siyo kwa kipindi flani ila katika Maisha yake yote ya hapa duniani,

“kimsingi mlei unaweza usielewe lakini Hakuna kazi yoyote njema na nzuri duniani ambayo haimuhusishi Padre moja kwa moja” Alisema Padre Asenga

Katika Hatua nyingine Padre Asenga alisema kuwa Malaika ni Rafiki wa Mungu lakini Padre ni muhudumu wa Mungu, hivyo yakupasa utambue kuwa mahusiano yako na Mungu yatazidi kuimarika endapo utaona na kueshimu kazi ya Muhudumu wa Mungu hapa Duniani ambaye ni padre.

“Mtakatifu yohane maria viane aliwai kusema endapo utaacha eneo kwa miaka kadhaa bila Padre watu wataanza Kuabudu wanyama” Alisisitiza Padre Asenga na kuongeza kuwa, Sote tuna bahati ya kuwa na mapadre na tuna kila sababu ya kufurahia zawadi hii kubwa ambayo Mungu ametupatia

 

Akihitimisha Homilia yake Padre Asenga Alimsihi padre Maendeleo kuendelea kudumisha upendo pamoja na kujenga tabia ya kuwasikiliza watu Zaidi, kwani Dunia ya Sasa imebadilika na ni tofauti na zamani ambapo Padre alionekana kujua kila kitu lakini Sasa watu wana uelewa mpana na hata wakati mwingine kuliko Mapadre hivyo ni wakati wa kumrudia Mungu katika maongozi ya watu wake

Kwa Upande wake Padre John Maendeleo, Aliwashukuru watu wote wenye mapenzi mema na wanao endelea kumtia moyo katika utume wake, huku akiwa ahidi maombi yake kila wakati, kwa Muda wote ambao atazawadiwa zawadi ya maisha na hatimaye Utakatifu.

“Ndugu zangu Ninawapenda sana, na ninatambua mchango wa kila mmoja aliyejitoa kwa hali na mali katika kuhakikisha ninafanikiwa katika utume wangu nikiwa kama padre, sina la kusema Zaidi ya Asante na Mungu Awabariki” Alihitimisha Padre Maendeleo

Na Izack Mwacha :Dar es Salaam


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE