Blog

  Leo Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Maria Magdalena wa Pazzi Bikira Mtakatifu huyu alizaliwa huko Florensi, mwka 1566 kwa Wazazi tajiri. Tangu aliporuhusiwa kukomunika,alipokuwa na umri wa miaka kumi, aliisogelea meza takatifu kila siku alipoweza . Aliingia Shirika la wakarmeli, akaishi maisha ya faragha akisali na kujinyima mambo mbalimbali. Maria Magdalena alizoea kusema: “Napenda Zaidi kuteswa […]

Wakristo Wakatoliki nchini, wametakiwa kumpokea Roho Mtakatifu ,ili wajazwe furaha, Amani na upendo, kama walivyo jazwa mitume siku ya Pentekoste na kunena lugha nyingine kama Roho alivyo wajalia. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Paroko wa parokia ya Mtakatifu MAURUS KURASINI, Jimbo kuu katoliki la DAR ES SALAAM, Padri FELIX MKUDE, wakati wa Adhimisho la […]

Leo Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Vincent wa Lereni Mtawa. Mtakatifu Vinsenti alikuwa mtu Msemaji na mwenye akili nyingi, akawa Askari kabla ya kuingia katika monasteria ya Lereni (Lerin,Ufaransa). Mtawa Vinsenti alipewa upadre,na mwaka 434 alitunga Kitabu kupinga uzushi uliotokea katika Kanisa. Katika Kitabu hicho alieleza kwamba yeye ni mgeni, mtu aliyeikimbia dunia na ubatili wake,kwa ajili […]

Waamini wa Kanisa Katoliki wameonywa kutowamiliki Mapadri na Mashemasi na kuwafanya kushindwa kutimiza vyema majukumu yao. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Askofu FLAVIAN KASSALA wa Jimbo Katoliki la GEITA wakati akitoa Daraja Takatifu la Ushemasi kwa FRATERI DIDAS KAHIGI katika Parokia Teule ya NYEHUNGE jimboni GEITA. Katika homilia yake Askofu KASSALA amesema kuwa, wajibu […]

Leo Mei 23 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Desideri wa Vienne Askofu na Mfiadini. Hatujui mambo mengi juu ya maisha ya Mtakatifu Desideri, ila inajulikana kwamba alikuwa Askofu wa Vienne huko Ufaransa. Pia alikuwa mmoja wa Maaskofu ambao Papa Gregori Mkuu alimwandikia amsaidie Mt.Augustino katika safari yake ya kwenda Uingereza kutoka Roma. Bidii aliyoionyesha Mtakatifu Desideri katika […]

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Anthony Lagwen kutoka Jimbo Katoliki la Mbulu, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Mbulu, nchini Tanzania. Askofu Mteule Anthony Lagwen alizaliwa tarehe 5 Julai 1967 huko Tlawi, Jimboni Mbulu. Baada ya masomo yake ya msingi, alibahatika kuendelea na masomo ya sekondari katika Seminari Ndogo ya Sanu, Jimbo […]

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la DAR ES SALAAM, Mwadhama POLYCARP KADINARI PENGO amewataka Vijana waliopokea Sakramenti ya Kipaimara kuyatumia vyema Mapaji SABA ya Roho Mtakatifu waliyoyapokea, na sio kuleta majivuno na mafarakano katika jamii. Kardinali PEGO ametoa wito huo jana katika Homilia yake, wakati akiadhimisha Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia […]

Leo Mei 22 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Rita wa Kashia, Mtawa. Mtakatifu Rita alizaliwa mwaka 1381 huko Kashia (itAlia). Alibatizwa akaitwa Margarita, tangu utoto wake aliazimia kumtumikia Mungu katika Konventi ya Mt. Austino huko Kashia, lakini alipokuwa na umri wa miaka Kumi na miwili, alilazimishwa na Wazazi wake na kuolewa na Kijana mmoja tajiri. Mume wake […]

Ee Mtakatifu Rita uliyeshiriki kimuujiza katika mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo pale msalabani, utujalie neema ya kuvumilia majaribu ya maisha haya kwa kujikatalia kitakatifu….Amina

Tumshukuru Mungu kwa zawadi ya Bikira Maria katika maisha yetu ya  kiroho. Kwa maombezi yake tujaliwe nasi kufika Mbinguni.


Current track
TITLE
ARTIST

CLOSE
CLOSE