Mtakatifu wa leo ni, Mt.MARGARETA wa HUNGARIA, MTAWA.

Written by on January 18, 2017

Leo tarehe 18 Januari, Kanisa linamkumbuka na kumheshimu Mtakatifu MARGARETA wa HUNGARIA, MTAWA.

Mtakatifu huyu alizaliwa mwaka 1242. Baba yake alikuwa mfalme wa Hungaria, ambaye alijenga konventi kwa ajili ya Masista wa Shirika la Mt. Dominiko huko Budapest, mji mkuu wa Hungaria. Mtakatifu Margareta aliishi maisha ya kujitesa sana kwa sababu alikuwa tayari hata kukatwa pua na midomo yake kuliko kukubali kutoka utumwani. Alikufa tarehe 18 Januari, mwaka 1270, akiwa ana umri wa miaka 28 tu.

Mtakatifu Margareta wa Hungaria, Mtawa, Utuombee…..Amina.


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE