Mhashamu Thelesphori Mkude amewataka vijana kuacha tabia kudharau na kuchagua kazi..

Written by on July 12, 2016

Askofu wa Jimbo Katoliki la MOROGORO Mhashamu THELESPHORI MKUDE, amewataka vijana kuacha tabia ya kudharau na kuchagua kazi na badala yake, Wafanya kazi kwa bidii ili waweze kujiletea maendeleo na taifa kwa ujumla.

Askofu MKUDE ametoa rai hiyo hivi karibuni wakati akifungua mkutanao mkuu wa nne wa Chama cha wafanyakazi wakatoliki (CWM) ulifanyika mkoani MOROGORO.

Amesisitiza kuwa kila Mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi, afanye kazi kwa ustawi wa nchi, ili kumuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dakta JOHN POMBE MAGUFULI, ambapo ana taka kila mmoja awajibike.

Aidha Askofu MKUDE amesema kuwa kufuatia utafiti uliofanyika hapa nchini, iligundulika asilimia 71 ya watanzania awafanyikazi huku wengi wakiwa Vijana, ambapo kisingizio walichonancho ni kudai hakuna ajira wakati si kweli, bali ni kudharau kazi.

Hata hivyo ameongeza kuwa nchi haiwezi kuendelea ikiwa wanao fanya kazi ni asilimia 29, kwani uchumi utakuwa chini na nchi itabaki omba mba wakati ina nguvu kazi yakutosha.

Chama cha wafanya kazi wakatoliki TANZANIA CWM kilianzishwa rasmi mwaka 2012 katika jimbo Katoliki la SONGEA na baadae na kuenea katika majimbo ya DAR ES SALAAM, BUKOBA, RURENGE_NGARA, MBINGA, MOROGORO na TANGA kwa lengo la kukuza imani, mshikamano, sauti ya wasio na sauti na kuimarisha uchumi katika ngazi ya familia.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE