Malaika wa Bwana:Likizo ni fursa ya kutafakari Neno la Mungu

Written by on August 8, 2017

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, wakati Kanisa Katoliki likiwa linaadhimisha Sikukuu ya Kung’ara kwa Bwana mawazo yake yameelekeza hasa  mapunziko katika kipindi cha kiangazi. Amewakumbuka watu wote walio na upweke, wagonjwa, wazee, masikini na watu wote waume kwa wake wanojinyenyekeza kutokana na ukosefu wa haki  msingi, nguvu na vurugu za ulimwengu huu.
Akianza tafakari la  somo la Injili amesema Domenika hii inaadhimisha sikuu ya kung’ara kwa Bwana . Injili ya siku inaelezea jinsi mitum Petro, Yakobo na Yohane walivyokuwa mashahidi wa tukio hilo, kwa maana, somo linasema: Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake, wakaongozana peke yao kwenda mlimani. Wakati wakiwa mlimani uso wake uling’ara kama jua na mavazi yake yakwa meupe kama nuru. Na tazama, waliona Musa na Eliya, akizungumza naye. Petro akamwambia Yesu, “Bwana tuko hapa, kama unataka, tujenge vibanda vitatu:kimoja kwa ajili yako, kimoja cha Musa na kimoja cha Eliya.” Wakati akisema hayo  ghafla  wingu zito likafunika. Baadaye  katika wingu  sauti ikasikika: Huyu ni Mwanangu mpendwa, niliyependezwa naye msikilizeni yeye. Baada ya wingu hilo Yesu alikuja akawagusa na kuwambia wasiogope.

 

Baba Mtakatifu ameendelea na tafakari, tukio la kung’aa kwa Bwana linatoa fursa ya ujumbe wa matumaini  kwa njia hiyo wote tutakuwa kama yeye aidha Injili hiyo inatualika kukutana na Yesu mwenyewe naadaye  kutoa huduma kwa ndugu. Kitendo cha mitume kutelemka kutoka mlimani, ni njia ya kutufanya kutafakari umuhimu wa kuondana na mambo ya kidunia ili kuweza kukamilisha  ule mwendo wa kumtafakari  Yesu. Hili ni jambo la kujiweka katika usikivu makini kwa ajili ya Kristo anayesali Mwana mpendelevu wa Baba Mungu, mwafaka wa  kusali. Ni kukijiweka kupokea vema kwa ukarimu na furaha Neno la Mungu.Katika kujiweka kiroho namna hiyo, yaani kuondokana na mambo ya kiumwengu , ndiyo njia tunayoitwa kuelekeleza ili kuweza kugundua  ukimya mkamilifu ndani mwetu, ambamo uboresha zaidi na kuendela kutafakari Injili na masomo ya Biblia

.

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea na tafakari akisema iwapo unaweka Biblia katika mikono yako na kukaa katika ukimya ndipo unapojisikia  uzuri wa ndani  na  furaha inaongezeka  kwa upya kutokana na neno la Mungu ndani yetu. Halikadhalika kwa mtazamo huo,katika kipindi cha kiangazi ni mwafaka ili kuweza kukua kiroho kwa kujikita zaidi katika shughuli za kutafuta na kukutana na Bwana. Katika kipindi hiki wanafunzi wako likizo wameondokana na shughuli zao za kila siku za masono na familia nazo  sasa wanatafuta kwenda likizo. Ni muhimu katika kipindi cha kupumzika  kuachana na shughuli za  za kawaida, kwamba kipindi hiki kiwe mwafaka kwao katika kutafakari  nguvu zao za kimwili na kiroho  ili wapate kijikita zaidi ndani ya roho zao.

 

Baada ya uzoefu wa maajabu ya kung’aa uso kwa Bwana  mitume wake walitelemka  wakiwa na macho na mioyo yao imebadilika kwa sababu ya kukutana na Bwana. Hiyo ndiyo njia inayoweza kufanywa na kila mmoja .Njia ya kugundua Yesu daima ni hai. Kuishi naye japokuwa inabidi pia kutelemka kutoka mlimani lakini tukiwa tumejaa nguvu za Roho wa Mungu ili kuweza kuamua njia moja,  sahihi yenye uhakika wa  uongofu pia wa kuwa mashuhuda kila wakati wa upendo ambao ni sheria ya maisha ya kila siku. Katika kubadilika kwa njia ya uwepo wa Kristo na kuwa na shahuku ya neno lake ndipo tutakuwa ishara ya upendo hai wa Mungu kwa ajili ya ndugu zetu  na hasa wale wanaoteseka, ambao mi pweke   na kubaguliwa. Kwa ajili ya wagonjwa na kwa ajili ya watu wengi waume kwa wake ambao  wako katika sehemu  za dunia wamenyenyekea kutokana na ukosefu wa haki,  wakisumbuka na mabavu na vurugu.

 

Katika kung’ara kwa Bwana ilisikika sauti ya Baba Mwenyezi ikisema, huyo ndiye mwanangu mpendwa msikilizeni yeye . Tutazama Maria Mama msikivu ambaye daima yuko tayari kusikiliza na kutunza  moyoni mwake kila Neno la Mtoto wake mpendwa. Tuwe na shuhuku ya Mama Maria mama yetu na Mama wa Mungu aweze kutusaidia kulishika neno la Mungu na yesu mwenyewe atatulinda ,aisha yetu.
Amemalizia akisema wamkabidhi  likizo zao hizo ziwe zenye utulivu na zaidi kwa wote ambao hawezi kwenda likizo kutokana na umri, sababu ya afya , au kazi na wengine  kutokana na uchumi na matatizo mengine yasiyo zuilika, aidha  kipindi hiki cha mapumziko uwe ni mwafaka  wa kuwa na marafiki pia kipindi kizuri.

 


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE