Makosa ya Makusudi katika Ndoa Hayakubaliki.

Written by on February 15, 2017

Askofu wa Jimbo Katoliki la RULENGE-NGARA Mhashamu SEVERINE NIWEMUGIZI, ametoa wito kwa Wanandoa wote kuwa, Mume au Mke asijifanye MSALABA kwa mwenzake tena kwa makusudi akidai kuwa eti ni kuvumiliana katika maisha.

Askofu NIWEMUGIZI ameyasema hayo katika ziara yake ya Kichungaji katika Parokia ya Mtakatifu THERESIA WA MTOTO YESU – BUHORORO wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ambapo amebariki Jozi 12 za ndoa.

Amesema Lengo la ziara hiyo ni kuangalia uhai wa IMANI, na namna Waamini wanavyoishi UKRISTO wao kama wanayoelekezwa na Mama Kanisa, kwani Alama ya kwanza ya maendeleo ya Kanisa ni kushiriki Sakramenti mbalimbali na hiyoi ndio sehemu ya uhai wa Imani.

Katika mahubiri yake Askofu NIWEMUGIZI amefafanua kuwa, tangu uumbaji Mungu alikuwa na mpango mzuri ila Mwanadamu akauharibu sababu ya tama mbaya za kuisikia sauti ya shetani.

Amewaeleza wana ndoa wote kuwa, Mungu anampa kila mmoja aina Fulani ya MSALABA ili aubebe hadi mwisho wa maisha yake, na Wokovu wa mtu ni MSALABA wake, huku akibainisha kuwa katika Ndoa kuna makosa ya makusudi ambayo yanafanyika ambapo mhusika anajua hali halisi, kwa mantiki hiyo hayakubariki katika maisha ya Ndoa kadiri ya makubaliano na Mambo muhimu yanayokubarika ni UPENDO na UAMINIFU katika Imani.

Hata hivyo Askofu NIWEMUGIZI ametoa wito kwa Waamini kujenga utamaduni wa kutunza kumbukumbu na takwimu za sensa ya waamini, ili kuwa rahisi kufanya tathimini ya maendeleo ya kiroho na kimwili.

 


Current track
TITLE
ARTIST

CLOSE
CLOSE