Maisha ya Mbinguni yana Anzia Duniani, kwa kuyanyima nafasi yaliyo ya kimwili.

Written by on October 27, 2017

Na Izack B Mwacha.

Wakristo wakatoliki Duniani waaswa kuishi Maisha ya Mbinguni wakiwa Hapa duniani, kwa kufanya yaliyomema ambayo yatapelekea Dunia kuwa na Amani na Mahali pazuri pa kuishi.

Hayo yamesemwa mapema hii leo na Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania Padre John Maendeleo, wakati wa Ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika pango la Bikira maria lililopo makao makuu ya Radio hiyo.

Padre maendeleo ameongeza kuwa ili uweze kuishi Maisha ya Mbinguni Ukiwa duniani ni Lazima ayape mambo ya Kiroho kipaumbele na siyo ya kimwili, Kwani mambo ya kimwili yakikutawala Huwezi kuishi kwa Amani.

Akifafanua zaidi Padre maendeleo Amesema kuwa ili uweze kufanikiwa kuishi Maisha ya Mbinguni Ukiwa duniani ni Lazima uyafanye mazoea ya kuyaishi Japo Yana changamoto zake ila Yana furaha na amani pia ukifanikiwa kuyaishi.

Hata hivyo amehitimisha kwa kusema kuwa mazoezi yanayoitajika kwa kiwango kikubwa ni sala na siyo vinginevyo, na huo ndio Mtihani wa Mwisho wa kuyaishi maisha ya mbinguni ukiwa duniani.


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE