Magufuli: Tutamkumbuka Askofu Chengula kwa kusimamia Ukweli.

Written by on November 26, 2018

DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI leo ameungana na Maaskofu, Mapadre, Watawa na Waamini wa Kanisa Katoliki kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA Mhashamu Askofu EVARISTO CHENGULA.

Misa Takatifu ya kumuaga Marehemu Askofu CHENGULA imeongozwa na Askofu Mkuu Mwandamizi JUDE THADAEUS RUWA’ICHI, katika Kanisa la Mtakatifu IMAKULATA lililopo Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu, KURASINI Jijini DAR ES SALAAM.

Akitoa salamu za pole baada ya Misa hiyo, Rais MAGUFULI amesema kuwa, pamoja na majukumu yake ya kutoa huduma za Kiroho Marehemu Askofu CHENGULA alisimamia ukweli ikiwemo kupinga hadharani ndoa na mapenzi ya jinsia moja licha ya kuwepo mashinikizo mbalimbali.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu FLAVIAN KASALLA, akitoa salamu kwa niaba ya Baraza amemshukuru Rais MAGUFULI kwa ushirikiano alioutoa wakati wa kuuguza, na baada ya kifo cha Askofu CHENGULA na pia amewashukuru madaktari na wauguzi, viongozi na wote waliokuwa wakimuombea kabla na baada ya kifo.

Askofu CHENGULA alifariki dunia Novemba 21, mwaka huu katika Taasisi ya Moyo ya JAKAYA KIKWETE Jijini DAR ES SALAAM alikokuwa akipatiwa Matibabu.

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE