Leo Septemba 14 Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Kukutuka kwa Msalaba

Written by on September 14, 2018

Leo Septemba 14 Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Kukutuka kwa Msalaba

Sisi Wakristo hatuna budi kuutukuza Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa sababu kwa njia yake ndipo tumekombolewa. Na hiyo ndiyo dhamiri ya Sikukuu ya leo. Ushindi na ukuu wa Msalaba  wake Bwana, tuyasome maneno yaliyoandikwa na Mt.Paulo katika barua zake kwa Wakristo.

“Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri habari njema , tena niihubiri bila kutegemea maarifa  ya hotuba  za Watu,  kusudu nguvu  ya kifo  cha Kristo Msalabani isibatilishwe. Maana ujumbe kuhusu kifo  cha Kristo Msalabani ni jambo la kipumbavu  kwa wale walio katika mkumbo  wa kupotea , lakini  kwetu sisi tulio katika  njia  ya wokovu  ujumbe  huo ni nguvu ya Mungu” (1 Kor 1: 17-18)

“Mimi  sitajivunia kamwe chochote  isipokuwa Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, maana kwa njia ya Msalaba  huo Ulimwengu umesulibiwa  kwangu, nami nimesulibiwa kwa ulimwengu” (Gal.6:14)

“Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya Wayahudi na Watu wa Mataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa Msalaba wake  aliziunganisha  jamii hizo kuwa moja, na  kuzipatanisha na Mungu” (Efe.2:14, 16)

“Alijinyenyekeza na Kutii mpaka  kufa, hata kufa Msalabani. Wako Watu  wengi ambao ni adui wa Msalaba wa Kristo, Mwisho wao ni Moto, kwani tumbo lao ndio Mungu wao, wanaona fahari juu ya mambo ambayo wangepaswa kuyaonea aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia. Lakini sisi ni raia wa Mbinguni, na twatazamia  kwa hamu kubwa Mkombozi  aje kutoka mbinguni , Bwana Yesu Kristo. yeye ataibadili  miili yetu  dhaifu inayokufa na kuifanya ifanane  na mwili wake mtukufu kwa nguvu ile ambayo  anaweza kuviweka vitu vyote chini ya Utawala wake” (Fil.3:18-21)

“ Kwa ajili ya furaha  iliyokuwa inamgojea, yeye alivumilia  kifo Msalabani, bila kujali juu yake, na sasa anaketi  upande wa kulia  wa kiti cha enzi cha Mungu.” (Ebr.21:2)

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE