Leo septemba 13 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Yohani Krisostomo Askofu na Mwalimu Wa Kanisa

Written by on September 13, 2018

 

Leo septemba 13  Kanisa linamkumbuka  Mtakatifu  Yohani Krisostomo Askofu na Mwalimu Wa Kanisa

 Yohani krisostomo alizaliwa Antiokia (Uturuki) Mwaka 349. ‘Krisostomo’ ni jina la Kupanga, maana yake ni “Mwenye mdomo wa dhahabu”, kutokana na mahuburi kadhalika na maandishi yake mengi yanayo ifafanua Imani na kuhimiza Maisha ya Kikristu. Baba yake alikuwa Mkuu wa majeshi aliye shujaa; Baba huyu alifariki dunia kabla Yohani hajapata kukua. Wakati huo, Mama alikuwa na umri wa miaka Ishirini tu. Igawa alikuwa bado kijana, aliamua kukaa katika hali ya ujane kwa maisha yake yote na kumlea vizuri mwanae. Akafanya mpango ili apate kufundishwa na Mwalimu mashuhuri.

 Yohani alipanga urafiki na mmoja wa Wanafunzi wenziwe, aliyekuwa akiitwa Basili. Kijana huyu alikuwa mwelevu sana. Kadhalika mwenye maadili mema, na alizidi kumvutia Yohani kwa mifano yake. Baada ya kufiwa na Mama yake, Yohani alijitenga na Watu, akakaa upweke pangoni,akiitunza Roho yake kwa Kusali na Kufunga. Katika muda huo wote, alikuwa ameisoma sana Biblia kiasi cha kuisema yote kwa moyo, akifanya Kozi ya Kichungaji kwa muda huo wa miaka kumi na miwili. Siku moja , aliteuliwa na Watu wa Konstantinopoli (Uturuki) ili awe Askofu wao. Ijapokuwa Yohani hakukitaka cheo hicho, Watu walimng’ang’ania tu, wakamchukua na wakamweka garini na kumpeleka kwao.

Ingawa alikuwa mtu mwenye cheo, mazoezi yake yaliendelea kufuata mtindo uleule wa zamani: alikula mara moja kwa siku, na kunywa maji tu; alilala kwa muda wa saa tatu au nne, na kusali kwa muda mrefu. Alikuwa na imani kubwa kwa sakramenti ya Ekaristi. Alilichunga kundi lake kwa bidii. Wakristu waliokuwa wema, waliimarishwa naye, na wale waliopuuza amri za Mungu aliwakaripia kwa uzembe wao. Watu walimsikiliza kwa makini na furaha kwa vile alikuwa Msemaji mashuhuri na mwenye moyo mwema. Lakini, wale waliokuwa wamekemewa naye kuhusu mwendo wao mbaya, walimwonea na kuchongea kwa Kaisari, Hasa adui yake alikuwa Eudoksia, mkewe Kaisari, ambaye alikuwa Mwanamke mwovu aliyeshirikiana na wafitini wa dini, kuwanyang’anya mali zao na kuwadhulumu raia wenye kudai haki yao.

Mara ya kwanza, askofu Yohani alipoondolewa na Kaisari kwenye madaraka ya Uaskofu na kuhaishwa kwa nguvu, wakristu walilalamika sana kiasi cha kuwashurutisha wakuu wao wamruhusu Askofu wao arudi kwao. Alipofukuzwa kwa mara ya pili, alikuwa amekaribia umri wa uzee. Hata Askari waliamuwa kumpeleka mbali na kumsumbua njiani kadiri walivyoweza ilia pate kufa upesi, Kwa hivyo, Askari hao walimlazimisha Askofu Yohani atembee kwa miguu, Kila siku, mwendo mrefu, mchana kutwa akiwa juani, katika njia mbaya, na wakati walipoamua kupumzika, walifanya hivyo tu katika Vijiji vile vidogo ambamo Askofu hangeweza kupewa huduma ya viburudisho. Hivyo, baada ya siku nyingi za mateso ya kila namna, ya njaa na kiu, Askofu Yohani akapata kufahamu ya kwamba nguvu zake zilikuwa zimemwishia. Alizimia njiani, akafa palepale, akisema “Tumsifu Mungu siku zote”. Huo ulikuwa mwaka 407. Umri wake ulikuwa miaka Sitini.

Watakatifu wengine wa leo ni Mt. FILIPUS, mfiadini; Mt. EULOGIUS, askofu wa Aleksandra; TEODOLUS, askofu mfiadini (Misri).

Haya ndio maisha ya Mtakatifu Mtakatifu  Yohani Krisostomo Askofu na Mwalimu Wa Kanisa kwa mujibu wa kitabu cha Watakatifu.

 

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE