Leo Novemba Kanisa linamkumbuka na kumheshimi Mtakatifu Wilibrodi,Askofu na Mtawa

Written by on November 7, 2018

Leo Novemba Kanisa linamkumbuka na kumheshimi Mtakatifu Wilibrodi,Askofu na Mtawa

Mtakatifu Wilibrodi, Mtume wa Uholanzi, alizaliwa Uingereza mwaka 658. Alipokuwa na umri wa miaka saba, Wazazi wake walimpeleka Shuleni katika Monasteria ,ili akasomeshwe.Toka hapo aliingia Utawani,na kwa Uongozi wa Walimu wenye akili aliendelea katika maarifa ya Dini kadhalika na katika maarifa mengine. Alipokuwa na umri wa miaka thelathini,alipadirishwa, akavuka bahari kwenda kuhubiri injili kwa watu wa Uholanzi.

Alijaliwa kuwaongoa watu wakawa Wakristu katika dini Katoliki, akajengesha Kanisa mjini Utrekt. Baadaye alisafiri kwenda Roma, na huko alipata Uaskofu kwa mikono ya Papa.

 

Mtakatifu Wilibrodi, baadaye akarudi Utrekt, ambako alijenga Kanisa. Na Baadaye,akaanzisha Monasteria mjini Echternach (Luksemburg), ambayo ndiyo yakawa makao yake na kitovu cha utendaji wa shuguli zake.

Mtakatifu Wilibrodi alifariki Dunia katika monasteria yake kule Echternach (Luksemburg), mnamo tarehe 7 Novemba mwaka 739. Alikuwa mzee mwenye umri wa miaka thamanini na moja. Hati,aliyoiandika yeye mwenyewe, ipo bado imehifadhiwa mjini Paris(Ufaransa), Ndani ya hati hiyo aliandika kwamba “alivuka Bahari ya Kaskazini mwaka 690,na kwamba aliwekwa Wakfu kuwa askofu mjini Roma mwaka 695.

 

Mtakatifu Wilibrodi, UTUOMBEE

 

 

 

 

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE