Leo Novemba 22 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Sesilia, Mfiadini (Karne ya Tatu)

Written by on November 22, 2018

Leo Novemba 22 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu  Sesilia, Mfiadini (Karne ya Tatu)

Mambo yanayojulikana kwa Hakika kabisa kuhusu Mt. Sesilia ni machache sana, nayo ni kwamba alikuwa Bibi aliyekaa Roma (Italia) Karne ya Tatu, na kwamba alijitahidi Kanisa lijengwe ambalo baadaye liliitwa ‘Kanisa Sesilia.’ Basi, ni hayo.

Sasa hadithi nzuri imetungwa juu ya Maisha yake njisi alivyoifia dini, nayo imeandikwa kwenye kitabu Kiitwacho Mateso ya Mt. Sesilia, ambacho kilimwonyesha yeye kuwa mfiadini ambaye aliuawa kwasababu ya upendo wake kwa Kristu. Sesilia alikuwa Binti wa jamaa tukufu ya Kiroma (Italia), aliigia Ukristu na aliweka Nadhiri ya ubikira ingawa Wazazi wake walikuwa wapangani. Baba na Mama yake walitaka kumwoza kwa nguvu kwa jamaa mmoja jina lake Valeriani. Sesila hakuweza kukimbia, alijiweka tayari kwa kufunga na Kusali ili apate msaada wa Mungu katika masumbuko yake. Siku ya Kuisherehekea harusi, watu wa nyumbani walipokuwa wakipokuwa wakipiga zumari na ngoma. Sesilia allimba rohoni mwake. “Ee Mungu wangu, uilinde roho na uulinde mwili wangu safi, nisitiwe haya mbele za watu”.

Usiku alipokutana kwa mara ya kwanza na mchuba wake, Sesilia alimwambia Valeriani: “Ninayo siri na sharti nikuambie. Karibu yangu husimama malaika mkuu anayenilinda. Ukiniacha bikira, atakupenda kama anavyonipenda mimi.” Valeriani alishtuka, Kisha akasema: “Nionyeshe basi malaika huyo.” Naye sesilia alimwitikia: “Utamwona ukibatizwa”. Kwa shauri la Sesilia Valeriani alikwenda kumwomba Papa Urbano kufundishwa naye, kisha akabatizwa. Baada ya Kubatizwa alirudi kwa sesilia. Kumbe, mara alimwona malaika karibu naye akinga’aa kama jua akishikilia mkononi mataji mawili ya maua, akaliweka taji moja kichwani kwa Sesilia, na jingine Kichwani kwake Valeriani.

Tibursi ndugu ya Valeriani aliposikia habari hii, akajisema kuwa naye ni mkiristu. Wote wawili walikamatwawakauawa. Liwali Almaki, aliwaza kwamba sasa ataweza kuwanyang’anya mali zao, lakini Sesilia ajkafanya haraka kuwagawia maskini fedha. Liwali alikasirika sana na akataka kumshurutisha Sesilia alijibu bila woga: “Afadhali nife kuliko kutoa sadaka kwa sanamu za maweau chuma”. Almaki akiogopa kwamba wangeanza kunfanyia fitina akatoa amri wampeleke Sesilia nyumbani kwake, wamfungie kwenye chumba cha mvuke wa moto kusudi wamzuie asipate kuvuta pumzi. Wakaitimiza amri hiyo, lakini sesilia akawa bado yu hai. Mwisho Liwali akamtuma mtesi huyo alimkata Sesilia kwa upanga mara tatu, lakini hakuweza kummaliza. Kwa kuwa ilikuwa imekatazwa kupiga zaidi ya mara tatu, akamwacha Sesilia pale pale amezimia. Alishida siku tatu katika hali hiyo, akivumilia kufa kwa mateso makubwa hayo.

Mt. Sesilia husemwa kuwa yeye ndiye somo wa waimbaji wa kanisa kwa maana Sesilia aliimba rohoni mwake wakati wapiga muziki walipokuwa wakicheza zumari na kupiga ngoma katika sherehe yaharusi yake na Valeriani. Tunapomkumbuka leo katika liturjia, tunawombea wale wote ambao huwa wanajitahidi kufanya ibada za Kanisa ziwe nzuri zaidi kwa muziki na nyimbo zao.

    

Watakatifu wa Afrika tarehe 22 Novemba

Mt. Maurus, mfiadini aliyetoka Moroko.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE