Leo Machi 1 Kanisa linamkumba Mtakatifu Switberti, Askofu

Written by on March 1, 2018

Leo Kanisa linamkumba Mtakatifu Switberti, Askofu

Maisha ya Switberti ni kielelezo bora kuhusu matatizo katika maisha ya wamissionari, matatizo ya usafiri katika nchi za misioni na vikwazo vilivyokuwepo kutokana na vita vya makabila ambayo wakati mwingine huharibu ushindi wa mwanzo wa kueneza Injili.
Switberti ni mmojawapo wa kikundi cha wamisionari kumi na wawili Waingereza na Waairishi walioongozwa na Mt.Wilibrodi (taz.7 Nonemba).Wamisionari hao walitoka Uingereza mwaka 690,wakavuka Bahari ya Kaskazini,wakaanza kueneza Injili kwa Wafrisi, kabila linaloishi Uholanzi na Ujerumani. Baadaye,walielekea upande wa kusini wakitembea umbali mrefu kwenye nchi kavu kwa kufuata mto Rain. Hii ilikuwa shuguli kubwa sana kwa wakati ule.Walipata shida nyingi ,na walivikabili vizuizi vingi,lakini mwishoni walifanikiwa,wakaanza kuhubiri na kufundisha katika sehemu zile.Mtakatifu.Switberti aliwaingiza watu wengi katika dini kwa utamu wa maneno yake.
Kwa sababu Wamisionari wenzake walimchangua kuwa askofu,Mtakatifu.Switberti aliamua kurudi Uingereza kutafuta Wamisionari wengi zaidi,na akiwa nyumbani alipewa daraja ya Uaskofu.Kabla ya kurudi Uingereza,alimwachia Mtakatifu.Wilibrodi kazi ya kuyaangalia makanisa aliyokuwa amekwisha kuyafungua.
Askofu Switberti aliporudi Ujerumani tena,baada ya kupewa Uaskofu,alipenya zaidi katika nchi na alibatiza watu wengi wa makabila mengine.Lakini kwa bahati mbaya sana,miaka michache baadaye kabila la wasaksoni waliteka na kuishikilia nchi na hivyo kazi yake iliharibiwa sana.
Askofu Switberti alikimbilia katika kisiwa kimoja huko mto Rain na kujitayarisha kwa kifo chake.Alijenga nyumba ya kitawa huko na alikufa hapohapo kwenye nyumba hiyo,mwaka 713.Masalia yake yaliwekwa kwenye sanduku ambalo baadaye lilipotea.Lakini baada ya miaka 900 likapatikana tena.Bado linahifadhiwa na kuheshimiwa,na miujiza mingi imetokea kwa heshima yake.

Mtakatifu Switberti, Askofu……UTUOMBEE.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE