Leo Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Ubaldo, Askofu wa Gubbio.

Written by on May 16, 2018

Leo Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Ubaldo, Askofu wa Gubbio.

Ubaldo alizaliwa katika ukoo bora huko Gubbio karibu na Asizi (Italia). Wazazi wake walikufa yeye akiangalia Mtoto, kwa hiyo alielimishwa na Mjomba wake aliyekuwa Askofu wa Gubbio. Kisha BAADA ya kumaliza mafunzo alipewa daraja la Upadre akawa Dekani wa Parokia . Alikuwa na kazi kubwa ya kuleta mabadiliko katika maisha ya Mapadre, akiwahimiza wakae pamoja kama jamii kwa hali moja. Mabadiliko hayo yalifanyika wakati Mt.Fransisko wa Asizi alipopitia huko Gubbio.
Miaka kadhaa baada ya mabadiliko yaliyoletwa na Padre Ubaldo, nyumba ya mapadre ilichomwa moto. wakati ule Ubaldo aliona ilikuwa vema aishi maisha ya upweke. Alikwenda kwa padre mmoja kamweleza Nia yake. Padre huyu alimshauri arejee Gubbio aendeleze kazi aliyoianza. Ubaldo alifanya hivyo, na alifanikiwa mara dufu. Mwaka 1228, PAPA alimchagua Ubaldo awe Askofu wa Gubbio. Alifanya kazi ya uaskofu vema kabisa zaidi ya miaka thelathini. Kama vile MT.Fransisko wa Asizi,alikuwa na Uvumilivu mwingi. Mara nyingi alitoa msamaha kwa wote waliomkosea. Aliwatetea watu hadharani.
Kaisari Frederiko Barbarossa katika vita yake huko Italia, aliuvamia mji wa Spoleto,na kisha alitishia kuivamia Gubbio. Lakini Askofu Ubaldo alimwendea na alifaulu kugeuza nia yake. Miaka mwili ya maisha yake Ubaldo aliteseka kwa magonjwa makali, lakini alivumilia yote hayo kwa ujasiri wake aliokuwa nao. Alifariki tarehe kama ya leo tarehe 16 Mei, mwaka 1160, na tunelezwa kuwa miujiza mingi ilitendeka kwenye kaburi lake. Na aliwekwa katika orodha ya waTakatifu mwaka 1192.

Haya ndio maisha ya Mtakatifu Ubaldo, Askofu wa Gubbio kwa mujibu wa Kitabu cha Watakatifu.
:Watakatifu wote wa Mungu. Mtuombee


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE