Kupanda mbegu siku zote ni kazi rahisi kuliko kuimwagilia: Kardinal NJUE

Written by on November 7, 2018

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la NAIROBI nchini KENYA, Kardinal JOHN NJUE ameeleza kuwa, kupanda mbegu siku zote ni kazi rahisi kuliko kuimwagilia na kuitumza ili iweze kukua, katika usahihi wake na kuwa na manufaa kwa vizazi vijacho. 

Kardinali NJUE amesema hayo jana katika homilia yake, wakati wa adhimisho la sadaka ya Misa Takatifu ya kilele cha maadhimisho ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara, ambapo amemwakilisha Baba Mtakatifu FRANCISKO kama mjumbe maalum katika maadhimisho hayo.

Katika homilia amebainisha kuwa Wamisionari walioileta Imani ya Kanisa Tanzania Bara, walijua fika hatari ya magonjwa pamoja na hatari nyinginezo za kibinadamu, lakini kupitia Sauti ya Mungu walikubali hata kufa kifo dini. 

Katika hatua nyingine Kardinali NJUE amewataka watu wote kuishi Maisha halisia na siyo kuiga Hali ya Maisha kwa kuonyesha kicheko kwa wanaocheka, ili na wewe uonekane mwenye furaha, kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unashindwa hata kuisikia Sauti ya Mungu pale atakapokuitaji.


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE