Kanisa Katoliki Tanzania la pata pigo

Written by on November 21, 2018

TANZIA

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (tec) Askofu Grevas Nyaisonga anatangaza kifo cho cha Askofu wa Jimbo katoliki la mbeya mhashamu evaristo chengula.

Kilichotokea Tarehe 21/11/2018 majira ya mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa anapatiwa matibabu.

Askofu Chengula alizaliwa Januari Mosi mwaka 1941 Kijijini Mdabulo na alipata Daraja Takatifu ya Upadri Oktoba 15 mwaka 1970 na mnamo novemba 8 mwaka 1996 alichaguliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya na kuwekwa Wakfu kama Askofu wa Jimboni hilo Februali Mbili mwaka 1997.

Askofu Chengula amelitumikia Kanisa kwa miaka 48 ya Upadri na Miaka 21 ya Uaskofu.

Radio Maria Tanzania itaendelea kukuletea taarifa kadili zitakavyokuwa zikitolewa na baraza la maaskofu katoliki tanzania (tec).

Habari ziwafikire

  1. Maaskofu wote baraza la maaskofu katoliki tanzania
  2. Mapadre wote na watawa wote wakike na wakiume
  3. Familia, ndugu, jamaa, na marafiki
  4. Wana jimbo katoliki la mbeya,

Uongozi wa Radio Maria Tanzania unatoa pole za dhati kwa baraza la maaskofu katoliki tanzania tec, wana jimbo katoliki la mbeya, ndugu, jamaa na wakristo wote tanzania kwa kuondokewa na mpendwa baba askofu chengula.

+Raha ya milele umpe eeeh bwana na mwanga wa milele umuangazie marehemu apumzike kwa amani+ AMINA.

 

 

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE