Jimbo Katoliki la Iringa lapata Mapadre wapya 13

Written by on August 9, 2018

 

Wakati huu Kanisa linapoadhimisha miaka 150 ya Uinjilishaji TANZANI Bara, Mama Kanisa anaendelea kupokea watendakazi katika shamba lake na hii leo kupitia Jimbo Katoliki la IRINGA amepokea Mapadre wapya KUMI na WATATU.

Sadaka ya Misa Takatifu kwa ajili ya Daraja Takatifu ya upadre imefanyika katika Viwanja vya KICHANGANI na imeongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu DAMIAN DALLU wa Jimbo Kuu SONGEA na Mhashamu Askofu TARCISIUS NGALALEKUMTWA wa Jimbo la IRINGA.

Katika homilia yake Askofu NGALALEKUMTWA, amesekuwa kila mmoja anapaswa kutambua kuwa KRISTO YESU ni mwalimu na kiongozi, na kwamba Baba wa Mbinguni   alimfanya KRISTO Mwanae kuwa kuhani ili kusudi wanadamu watakaswe uovu wao na uhalifu wao.

Amesema kuwa KRISTO alifanya utakaso huo, upatanisho pamoja na marekebisho kwa mwadamu kupitia kujitoa kwake mwenyewe juu ya MSALABA na kuwa kuhani, altare na mwanakondoo.

Adhimisho hilo la Misa Takatifu ya Daraja ya Upadre limekwenda sanjari na kumpongeza Askofu TARCISIUS NGALALEKUMTWA kwa kutimiza miaka 25 tangu ameanza kuliongoza  Jimbo la IRINGA.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE