“Ishini maisha yampendezayo Mungu, ili majina yenu yaandikwe katika kitabu cha walio hai”. Askofu Ngalalekumtwa

Written by on March 1, 2018

Wakristo Wakatoliki nchini wametakiwa kutenda yaliyomena kulingana maandiko matakatifu, pamoja na kuziishi ahadi zao za ubatizo na kipaimara, ili siku ya mwisho watakapo aga dunia wakute majina yao yameandikwa katika kitabu cha walio HAI.

Wito huo umetolewa na Askofu TARCISIUS NGALALEKUMTWA wa Jimbo Katoliki la IRINGA katika mahubiri yake wakati akiadhimisha Misa Takatifu ya maziko ya Padre FRANSIS MKAKANZE aliye kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kibao Jimbo Katoliki la IRINGA.

Katika Misa iliyofanyika Parokia ya TOSAMAGANGA Jimboni humo Askofu NGALALEKUMTWA, amesema kuwa kila mwamini anapaswa kulitafakari hilo, na hasa wakati huu wa kipindi cha KWARESIMA, kwani Mwenyezi Mungu anamgeuza ili awe kiumbe bora kwa vile anampenda.

Akimzungumzia Padre MKAKAZE, amesema kuwa wakati wa uhai wake ameweza kuiishi imani yake ya Kanisa Katoliki kwa maneno na vitendo, na hivyo hana wasiwasi maana jina lake tayari limeisha andikiwa katika kitabu cha walio HAI.

Wakati huo huo amewaomba Waamini kusali na kumwombea Padre MKAKAZE, ili Mwenyezi Mungu ampe tuzo anazostahili ikiwemo kukaa na wenye haki katika jiji la YERUSALEMU ya mbinguni, huku pia waendelee kuyaenzi mema yote aliyotatenda wakati akitoa huduma kwao.

Padre MKAKANZE alifariki Dunia ghafla Februari 24, Parokiani KIBAO na kuzikwa Februari 27 katika makaburi ya Mapadre huko TOSAMAGANGA Jimboni IRINGA.

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE