Dhamani Ya Maisha ni furaha ambayo ni wewe mwenyewe.

Written by on April 12, 2018

Imeelezwa kuwa ili kuishi maisha marefu yenye amani na upendo ni lazima uwe na furaha ya moyo ambayo inasababishwa na wewe mwenyewe.

Hayo yamesemwa na padre John Maendeleo Ambaye ni mkurugenzi wa matangazo Radio Maria Tanzania, Wakati akiwa katika kipindi cha katekisimu katoliki shirikishi, kinachorushwa na Radio hiyo kila siku ya juma tatu mpaka alhamisi majira ya saa tatu kamili asubui mpaka saa nne kamili asubuhi.

Akizungumza kuhusu Furaha, Padre Maendeleo amesema kuwa, Furaha ni Mlipuko wa Kicheko, au kitulizo cha Ghafla anachokipata Mtu Nafsini mwake, huku akiongeza kuwa sababu ya furaha ni mtu binafsi kama akiamua kuishi furaha yenyewe na kusisitiza ya kuwa, Endapo utafanya Maamuzi ya kuishi kwa furaha, huwezi kukasirika hata siku moja kwani tayari unakuwa umeijenga ndani yako.

 


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE