matukio

Page: 2

Mtakatifu  Sava  alizaliwa Mwaka  1175 akiwa mtoto wa kiume watatu wa Stefano wa Kwanza , Mfalme wa Serbia. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba alijiunga na wamonaki  wa Mlima  Athos ,(Ugiriki). Mt. Sava…Utuombee…Amina.

Mt. Hilari alizaliwa na wazazi matajiri wa  Akwitania waliokuwa wapagani.Alipokuwa naumri wa miaka thelathini na mitano aliongoka na kuwa mkristu kwa kusoma injili takatifu.Hatimaye aliteuliwa kuwa Askofu wa Pwatye mwaka 350. Mt. HilariwaPwatye….utuombee…Amina.

Mt. TeodosializaliwaKapadokia ,Uturuki.Alipokuwa kijana alikwenda kuhiji katika nchi Takatifu. Alipofika huko akatamani kukaa upweke iliapate kumtumikia Mungu. Mt. Teodosi…utuombee…Amina.

Mtakatifu William wa Burje, Askofu , tangu wakati wa utoto wake alimwelekea Mungu. Aliingia Upadre akamtamani Mungu zaidi na zaidi. Kwa nia hiyo  ndipo akakusudia  kujitenga na malimwengu. Mtakatifu William wa Burje, Askofu ……Utuombee……Amina.

Mtakatifu Adriano, Abati wa Kanterberi kwa asili alikuwa ni Mwafrika.Alifundisha sana kwa muda wa miaka 39, Kigiriki  na Kilatini, Maandiko Matakatifu na hasa Fadhila.Akafariki  dunia, tarehe 9 Januari mwaka 710. Mtakatifu  Adriano, Abati wa Kanterberi…….Utuombeee…..Amina

Mtakatifu Abo, Mfiadini , alizaliwa huko Bagdad nchini Iraq. Alikuwa Kijana Mwarabu na Muislam. Alibadili dini mara baada ya kubatizwa na kuwa Mkristo, hali iliyompelekea kufikishwa mbele ya Hakimu wa Kiislam na kukubali kuwa ameasi. Baada ya kukaa kifungoni kwa muda mfupi, walimkata kichwa. Mtakatifu Abo, Mfiadini……..Utuombee…….Amina.

Mtakatifu  Raymond , Padre, alizaliwa Mwaka 1175 huko Penyafort, Hispania. Alijifunza  Sheria za Kanisa katika Chuo  cha Bolonya( Italia). Wakati alipokuwa na umri wa miaka 47  aliingia Shirika la Mt. Dominika na alikuwa  Mhubiri hodari sana. Mtakatifu Raymond wa Penyafort, Padre….Utuombee!

Mungu Awabariki.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katokili la SONGEA Mhashamu DAMIAN DALLU amewataka Wakristo Wakatoliki kuwa watu wa kuomba msamaha pale wanapokosewa, pia kuwa tayari kutoa msamaha kwa kwa wengine. Askofu Mkuu DALLU amesema hayo mwishono mwa wiki wakati wa adhimisho la misa takatifu la kufunga mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya HURUMA YA MUNGU, ambapo misa hiyo […]

Wakristo Wakatoliki nchini wameaswa kuchangamkia mambo ya kanisa zaidi na siyo ya Mwalimwengu ili waweze kuishi maisha Matakatifu na ya kumpendeza Mungu, na kuzingatia utakatifu kama wito wa kila MBATIZWA. Wito huo umetolewa na Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la MWANZA Mhasham YUDATHADEUS RUWA’ICHI Katika homilia yake kwenye Adhimisho la Ibada ya misa takatifu […]


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE