habari

Page: 3

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la DAR ES SALAAMA Mwadhama POLYCARPY Kardinali PENGO, amewataka Wakristo kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu ili aendelee kuteua Watu ambao wataendeleza shughuli za Uinjilishaji katika siku za mbeleni. Kardinali PENGO ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika Ukumbi wa mikutano uliopo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu YOSEFU […]

Leo Oktoba 10 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu  Fransisko wa Borjia, Padre Fransisko alizaliwa Hispania mwaka 1510, Baba yake alikuwa Mkuu wa Mkoa. Baada ya kusoma chuoni, akiwa mwenye umri  wa miaka Kumi na Nane, alipewa kazi kwenye Ikulu ya Mfalme. Mwaka mmoja baadaye akafunga ndoa, na mke wake alimzalia Watoto wanane. Kama vile alivyokuwa Baba yake […]

  Wakristo Wakatoliki wametakiwa kusameheana wao kwa wao katika na hasa wakati huu Kanisa la TANZANIA linapoadhimisha Jubilei ya miaka 150 ya Uminisonari, ili kuwa huru kutoka katika utumwa wa Shetani. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la DAR ES SALAAM Mhasham EUSEBIUS NZIGILWA wakati wa Adhimisho ya Sadaka ya […]

Leo Oktoba 3 Kanisa linamkumbuka  Watakatifu Ndugu Ewaldi Hao ndugu Wawili wa tumbo moja,Waingereza wenye jina lilelile moja Ewaldi.   Lakini kwa kuwa rangi ya nyewele zao ilikuwa tofauti,mmoja aliitwa Ewaldi Mweusi,na mwezake Ewaldi Mweupe. Baada ya kukua na kusomea teolojia,walipadirishwa.  Muda mfupi tuu baada ya Mt.Wilibrodi na wenzake kutoka Uingereza mwaka 690, ili kufanya kazi […]

Leo Oktoba 2 kanisa linadhimisha kumbukumbu ya Malaika  Walinzi Wetu. Mungu kwa wema wake , ametupa sisi Malaika moja wa kutulinda tangu siku ya kuzaliwa kwetu mpaka saa ya kufa kwetu . watu wote, Watakatifu kwa wakosefu ,kila mmoja ana Malaika wake mlinzi. Malaika Mlinzi wetu hutuepusha na hatari zote, hutunza Roho zetu hutukinga zaidi […]

Leo Septemba 27 Kanisa linamkumbuka  Mtakatifu Vinsenti wa Paulo Padre na Mwanzilishi wa Shirika Mtume huyu wa Mapendo ya kindugu alizaliwa mwaka 1581 katika nchi ya Ufaransa.   Wazazi wake walikuwa wakulima,na alipokuwa bado Mtoto, Baba  yake alizoea kumtuma Vinsenti kuchunga mifugo yao malishani.   Toka Utoto wake alikuwa na tabia njema ya kuwahurumia maskini, alipowahi kuwakuta […]

Leo Septemba 26 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Watakatifu Kosma na Damiano,Wafiadini Hatujui  mengi kuhusu maisha yao.  ila  Inasemekana kwamba Kosama na Damiano walikuwa ndugu wa Tumbo moja.   Walijifunza utabibu ili wapate ruhusa ya kuingia katika nyumba za wapagani,na kuwaongoa kwa dini ya Yesu Kristu.  Walipowaponya wagonjwa bila kudai ada kama malipo  watu waliwaita ‘’Watakatifu bila fedha’’. […]

  Na Izack Mwacha: Iringa Askofu wa Jimbo katoliki la Iringa Mhasham Tarcisius Ngalalekumtwa Amewataka waamini kutambua ya kuwa, hakuna mtu mwenye uwezo wa kusema au kuelezea sifa zinazomuhusu Mama Bikira Maria kwa ukamilifu wake, kwani Mama huyo ni kiumbe safi, teule na jirani wa Yesu.   Askofu Ngalalekumtwa Ameyasema hayo mwishoni mwa juma wakati […]

  Na Izack Mwacha: Dar es salaam Wito umetolewa kwa Wanaume wote walioko ndani ya Ndoa kuwapikia wake zao jambo ambalo litaonyesha alama ya upendo pamoja na kujijengea utaratibu mzuri wa kuzilisha familia zao Wito huo umetolewa na padre Edward Ijengo wa jimbo katoliki la Kondoa wakati akiadhimisha ibada ya misa takatifu dominika ya 25 […]

Leo Kanisa linakumbuka Mtakatifu  Visenti  Strambi , Askofu Vinsenti Strambi alizaliwa 1 Januari 1745 katika mji wa Sivita Venchia (Italia).   Alikuwa kitindamimba kati ya watoto wanne ambao Watatu wao walifariki wakiwa bado wachanga. Baba yake alikuwa mfanyabiashara ya madawa. Alikua tajiri,kwa hivi alijulikana sana.  Wazee wake waliutambua wajibu wao wakumlea vizuri mtoto wao,na Mama  yake,kama […]


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE