Kanisa

Page: 5

  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la DAR ES SALAAM Mwadhama POLYCARP Kardinali PENGO, amesema kuwa Maaskofu wote wanapaswa kutumikia nafasi zao kwa Waamini wa maeneo yote bila kujali sehemu anakotoka au aliozaliwa. Kardinali PENGO amesema hayo jana katika adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki […]

  Wakati huu Kanisa linapoadhimisha miaka 150 ya Uinjilishaji TANZANI Bara, Mama Kanisa anaendelea kupokea watendakazi katika shamba lake na hii leo kupitia Jimbo Katoliki la IRINGA amepokea Mapadre wapya KUMI na WATATU. Sadaka ya Misa Takatifu kwa ajili ya Daraja Takatifu ya upadre imefanyika katika Viwanja vya KICHANGANI na imeongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu […]

Wakristo Wakatoliki wametakiwa kuwapenda, kuwathamini na kuwaombea Mapadre na si kutengeneza chuki miongoni mwao. Wito huo umetolewa leo na Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA Mhashamu EVARISTO CHENGULA katika Adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu ya Upadrisho kwa Padre XAVERY MAFWIMBO, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu PATRICE VWAWA, jimboni humo. Askofu CHENGULA amesema kuwa, kitendo […]

Leo kanisa  linamkumbuka  Mtakatifu Dominiko Guzman Mtawa na Mwanzilishi wa Shirika Dominiko alizaliwa Hispania mnamo mwaka 1170.  Alijifunza teolojia,halafu alipata Upadre na akawa Naibu wa Mkuu wa nyumba ya Utawa.   Jambo lililoleta badiliko kubwa katika maisha ya Dominiko ni lile lililotokea wakati wa safari yake aliyoifanya pamoja na Askofu wake huko Ufaransa ya Kusini.  Katika […]

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI leo Agosti 7, 2018 amefanya mazungumzo na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) pamoja na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) walioomba kukutana nae na kujitambulisha, Ikulu Jijini DAR ES SALAAM. Viongozi wa TEC waliokutana na Rais MAGUFULI ni Rais wa Baraza […]

  Wakristo Wakatoliki nchini, wameshauriwa kuwa na KIU na NJAA ya mambo yadumuyo katika IMANI yao, na si kutamani mambo ya muda mfupi. Ushauri huo umetolewa na Padri RAFAEL MARIJITE Paroko wa Parokia ya Mtakatifu MARIA IMMAKULATA-BIHAWANA Jimbo Kuu katoliki la DODOMA, wakati akitoa tafakari ya Masomo Dominika ya 18 ya mwaka B wa kanisa […]

Wamini na Watanzania kwa ujumla wamehimizwa kutumia vyema Teknolojia ya habari na mawasiliano, hasa mitandao ya kijamii kwa manufaa ya kuhabarisha, kuleta Amani na  maendeleo katika Jamii badala ya kusambaza uzushi na kuleta mifarakano. Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la MWANZA Mhashmu YUDA TADEI RUWAICHI, ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Askofu […]

  Watawa nchini wamehimizwa kuishi maisha ya Umisionari na Uinjilishaji, kwa kuziishi Nadhiri TATU hasa UMASKINI, UTII na USEJA ili kuepukana na tamaa ya fedha na mali zinazopelekea kupotea kwa uchaji katika maisha ya Wito Mtakatifu. Wito huo kwa Watawa umetolewa na Padre GODFREY MSUMANGE wa Shirika la Wamisionari wa KONSOLATA, katika sadaka maalum ya […]

   Leo Aagosti 7  Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Siksto wa pili, Papa na Wenzake Wafiadini Siksto alizaliwa Atene,mji mkuu wa Ugiriki.   Alikuwa mwalimu mwenye hekima.   Alikuwa Padre na aliwekwa wakfu awe Askofu huko Roma mwaka 257. Zamani hizo alikuwa akitawala Kaisari Valerino,naye alikuwa adui na mtesi mkubwa wa wakristu.  Wakristu waliokataa kuabudu sanamu za uwongo waliuawa […]

Leo Agosti 2 Kanisa linakumbuka Mtakatifu  Eusebi  wa Verseli, Askofu Eusebi alizaliwa katika kisiwa cha Sardinia karibu na Italia,mwaka 286. Baba yake aliuawa kwa sababu ya dini wakati wa dhuluma ya Dioklesiano . Mama yake alipoachwa mjane ,aliwachukua Eusebi na dada zake ,wangali bado Watoto wadogo wote wawili,akaenda Roma ambapo Eusebi alipata elimu ya upadre. […]


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE