Kanisa

Mapadre Mapadri Watatu wa Jimbo Katoliki SAME ambao vifo vyao vilipishana kwa siku moja moja yamefanyika katika Seminari ndogo ya CHANJARE Jimboni SAME mkoani KILIMANJARO. Mapadre hao ni Padri MICHAEL KIRAGHANJA aliyefariki dunia Aprili 11 akiwa kwenye mafungo huko MAUA MOSHI, Padre AROBOGASTI MNDEME wa Parokia ya KIRANGARE alifariki Aprili 12 katika Hospitali ya Rufaa […]

Leo Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Marselino wa Embrun,Askofu Mtakatifu Marselino,anaheshimika kama Askofu wa kwanza wa Embrun (Ufaransa),alikuwa mzaliwa wa Afrika ya Kaskazini. Yeye na wenzake wawili,watakatifu Vinsenti na Damiano,walijitosa katika kuihubiri Injili huko Ufaransa. Walitua huko Nice (Ufaransa), kisha waliendelea Kusafiri mpaka Milimani. Eusebi wa Verseli aliyekuwa amefukuzwa huko alimweka Marselino wakfu na kumsimika awe Askofu […]

Leo Aprili 17 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Stefano Harding, Abate Mtakatifu Stefano Harding alizaliwa Uingereza akasoma katika chuo cha Monasteri ya Sherbo (Uingereza). Alisafiri na rafiki yake mmoja kwenda Roma. Wakati wa kurudi wakaona njiani vibanda duni kadhaa. Huko walikaa Mamonaki waliokuwa wakiishi maisha ya ufukara. Nusu ya muda wao walitumia katika kusali, nusu nyingine kwa […]

Leo Aprili 13 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Martino wa Kwanza Papa na Mfiadini. Martino alizaliwa Todi (Italia). Alichaguliwa kuwa Papa mwaka 649. Zamani zile Wamonoteliti wafitini wa dini,walijaribu kutangaza kokote mafundisho yao kwamba Yesu Kristu hakuwa na utashi wa kibinadamu. Katika mtaguso wa Laterani ilithibitishwa kwamba Kristu alikuwa na tashi mbili;utashi wa kibinadamu na utashi wa […]

  Leo Kanisa linamkumbuka na kumheshimu Mtakatifu Zeno ambaye alikuwa Askofu na Yosefu Moskati Mganga. Mtakatifu Zeno alizaliwa Afrika ya Kaskazini, alisoma sana Falsafa ya siku zile, mnamo mwaka 362 aliwekwa Wakfu kuwa Askofu wa Verona nchini Italia. Mtakatifu Zeno aliishi sana maisha ya kimaskini, na alikuwa akiwahimiza sana mapadre na Watawa wengine wajitolee. Makatifu […]

Tanzia. Kwa majonzi makubwa Mhashamu Baba Askofu Rogath Kimaryo anatangaza vifo vya mapdri wawili, ambao ni Padre Michael Kiraghenja, aliyefariki usiku wa kuamkia jana tarehe 11.4.2018, huko Maua Retreat House, alikokuwa kwenye mafungo. Na Padri Aribogasti Naimani Mndeme, kilichotokwa tarehe 11.4.2018. Katika hospital ya KCMS Moshi, alikokuwa anapatiwa matibu. Maziko ya mapadri hawa yatafanyika kwa […]

Leo Aprili 11, Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Stanislaus, Askofu na mfiadini na Mtakatifu Gema Galgani. Stanislaus alizaliwa Polandi mwaka 1030. Wazazi wake walikuwa Watu wa asili bora na matajiri. Walikaa muda wa miaka Ishirini bila kupata Mtoto, lakini mwishowe walijaliwa na Mungu kuzaa mtoto wa kiume, ambaye walimwita Stanislaus. Mtoto huyu alipewa Upadre mwaka 1070 na […]

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.JOHN POMBE MAGUFULI amesema, Serikali yake itaendelea kushirikiana na madhehebu yote ya Dini nchini katika nyanja zote, ili kuhakikisha kuwa amani iliyopo inaendelea kutunzwa kwa maendeleo ya Taifa na Wananchi wake. Rais MAGUFULI amesema jana katika hotuba yake wakati wa Misa Takatifu ya kumsimika rasmi Askofu Mkuu ISAAC AMANI, kuwa […]

Leo Aprili  10 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Fulberti, Askofu. Tunajua kutokana Na barua za Mt.Fulberti mwenyewe kwamba alikuwa wa ukoo usijulikana sana, nay a kwamba alizaliwa Italia na kukulia huko. Baadaye alienda Ufaransa kusoma. Alipohitimu akateuliwa kuwa msimamizi wa shule za kanisa kuu la Shartre (Chartres,Ufaransa). Kwa ajili ya juhudi zake,shule hizo zikawa maarufu sana katika […]

Leo Aprili 9, Kanisa kinamkumbuka Mtakatifu Walitruda. Waltruda ambaye familia yake ilikuwa mashuhuri sana, ni Msimamizi wa mji wa Mons katika Ubeligiji. Wazazi wake Walbert na Bertila, Dada yake Aldegonda, Mumewe Madelgari na Watoto wao wanne, Landri, Dentelini, Adeltruda na Madelberta,wote hawa huheshimiwa kama Watakatifu. Siku moja Mumewe Madelgari aliondoka akaingia katika Monasteria ambayo alikuwa […]


Radio Maria Tanzania

Current track
TITLE
ARTIST

CLOSE
CLOSE