Kuinjilisha

    Leo 14 Agosti Kanisa linamkumbuka Mtakatifu  Maksimiliani Koble,Padre na Mfiadini.  Maksimiliani Koble, alizaliwa  nchini Poland mwaka 1894 kama  Mtoto wa pili  wa Julius Koble na mke wake Maria,na alipobatizwa  alipewa jina  la Raymundi. Mama yake  alifaulu kuwalea  kikristu  kabisa watoto  wake  wote  na kuwaamshia  fadhila Alipofikia  umri wa miaka kumi,alizoea  kwenda  Kanisani  mara nyingi  […]

  Wakristo Wakatoliki Ulimwenguni kote  wametakiwa kufahamu kuwa, Mama BIKIRA MARIA aliyepalizwa Mbinguni  ni  MKRISTO  wa kwanza  kuishi maisha ya Imani,  na Utukufu, na  amepewa   heshima  kuu  kuwa Mama wa Mkombozi na mama  wa Mataifa  yote Duniani. Hayo yamebainishwa na Padre DOMINIC MWALUKO  Mmisionari  wa Shirika  la Damu Azizi ya YESU Provinsi ya TANZANIA  wakati […]

  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la DAR ES SALAAM Mwadhama POLYCARP Kardinali PENGO, amesema kuwa Maaskofu wote wanapaswa kutumikia nafasi zao kwa Waamini wa maeneo yote bila kujali sehemu anakotoka au aliozaliwa. Kardinali PENGO amesema hayo jana katika adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki […]

  Wakati huu Kanisa linapoadhimisha miaka 150 ya Uinjilishaji TANZANI Bara, Mama Kanisa anaendelea kupokea watendakazi katika shamba lake na hii leo kupitia Jimbo Katoliki la IRINGA amepokea Mapadre wapya KUMI na WATATU. Sadaka ya Misa Takatifu kwa ajili ya Daraja Takatifu ya upadre imefanyika katika Viwanja vya KICHANGANI na imeongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu […]

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican. Baba Mtakatifu Francisko asema,jangwa la maisha ya binadamu au udhaifu na mapungufu ya binadamu ni mahali pa kukutana na huruma, upendo na nguvu ya Mungu inayomwokoa mwamini na kishawishi cha kuabudu miungu vitu na watu! Waamini wanapaswa kutambua kwamba, Mungu aliye hai ni chanzo cha maisha ya […]

Wakristo Wakatoliki wametakiwa kuwapenda, kuwathamini na kuwaombea Mapadre na si kutengeneza chuki miongoni mwao. Wito huo umetolewa leo na Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA Mhashamu EVARISTO CHENGULA katika Adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu ya Upadrisho kwa Padre XAVERY MAFWIMBO, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu PATRICE VWAWA, jimboni humo. Askofu CHENGULA amesema kuwa, kitendo […]

Na Frt. Karoli Joseph AMANI  wa Jimbo kuu Katoliki Tabora. – Vatican.   Jumapili ya Matawi, vijana 12 walimkabidhi Papa Francisko Hati ya Utangulizi wa majadiliano yao, yaliongozwa na kauli mbiu ‘’Vijana, Imani na mang’amuzi ya miito’’. Hati hii ni sehemu ya Hati ya kutendea kazi (Instrumentum laboris) kwa ajili ya majadiliano wakati wa Sinodi […]

Leo kanisa  linamkumbuka  Mtakatifu Dominiko Guzman Mtawa na Mwanzilishi wa Shirika Dominiko alizaliwa Hispania mnamo mwaka 1170.  Alijifunza teolojia,halafu alipata Upadre na akawa Naibu wa Mkuu wa nyumba ya Utawa.   Jambo lililoleta badiliko kubwa katika maisha ya Dominiko ni lile lililotokea wakati wa safari yake aliyoifanya pamoja na Askofu wake huko Ufaransa ya Kusini.  Katika […]

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI leo Agosti 7, 2018 amefanya mazungumzo na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) pamoja na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) walioomba kukutana nae na kujitambulisha, Ikulu Jijini DAR ES SALAAM. Viongozi wa TEC waliokutana na Rais MAGUFULI ni Rais wa Baraza […]

  Wakristo Wakatoliki nchini, wameshauriwa kuwa na KIU na NJAA ya mambo yadumuyo katika IMANI yao, na si kutamani mambo ya muda mfupi. Ushauri huo umetolewa na Padri RAFAEL MARIJITE Paroko wa Parokia ya Mtakatifu MARIA IMMAKULATA-BIHAWANA Jimbo Kuu katoliki la DODOMA, wakati akitoa tafakari ya Masomo Dominika ya 18 ya mwaka B wa kanisa […]


Current track
Title
Artist

CLOSE
CLOSE