habari

Baraza la Ushauri la Jimbo Katoliki Mbeya limemchagua Naibu Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA, Padre FRANCIS MAGALLA kuwa msimamizi wa Jimbo hilo baada ya kufariki Askofu Evaristo CHENGULA hadi hapo atakapoteuliwa Askofu mwingine. Padre Magalla aliteuliwa na Askofu Chengula kuwa Naibu wake tangu  alipotangazwa kuwa Askofu wa Jimbo la Mbeya baada ya kuteuliwa na […]

RIPOTI KUU YA KAPU LA MAMA 2018 Bonyeza Link Ifuatavyo ili Kufuatilia Matokea ya Kampeni ya Kapu la Mama 2018, kama yalivyosomwa kwenye Ripoti Kuu.

MBEYA Vilio na Simanzi na majonzi vimetawala  kwa Mapadre, Watawa wa Kike na wakiume pamoja na Waamini wa Kanisa Katoliki Jimbo la MBEYA wakiwemo Wananchi mbalimbali wa ndani na nje ya Mkoa wa MBEYA mara baada ya kuwasili mwili wa Askofu CHENGULA (IMC) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa SONGWE. Mwili wa Askofu CHENGULA […]

  Leo Novemba 26 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Yohana Berkamans Mtawa. Yohani alizaliwa katika kijiji cha Diest (Ubelgiji) mwaka 1599, katika familia ya watu wenye kumcha Mungu. Baba yake alifanya kazi ya kushona viatu, lakini kazi hiyo haikumpatia masilahi ya kutosha. Hivyo Yohani aliyetaka kuwa Padre, baada ya kujifunza Kilatini kwa muda wa Miaka Mitatu, aliambiwa […]

DAR ES SALAAM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI leo ameungana na Maaskofu, Mapadre, Watawa na Waamini wa Kanisa Katoliki kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA Mhashamu Askofu EVARISTO CHENGULA. Misa Takatifu ya kumuaga Marehemu Askofu CHENGULA imeongozwa na Askofu Mkuu Mwandamizi JUDE THADAEUS […]

Leo Novemba 22 Kanisa linamkumbuka Mtakatifu  Sesilia, Mfiadini (Karne ya Tatu) Mambo yanayojulikana kwa Hakika kabisa kuhusu Mt. Sesilia ni machache sana, nayo ni kwamba alikuwa Bibi aliyekaa Roma (Italia) Karne ya Tatu, na kwamba alijitahidi Kanisa lijengwe ambalo baadaye liliitwa ‘Kanisa Sesilia.’ Basi, ni hayo. Sasa hadithi nzuri imetungwa juu ya Maisha yake njisi […]

  Askofu wa Jimbo Katoliki SUMBAWANGA Mhashamu BEATUSI URASA amewataka Vijana kuishi misingi ya Kanisa Katoliki, kwa kujitoa kufanya kazi kikamilifu na uaminifu, ili kuliletea Kanisa na Taifa Maendeleo. Askofu URASA amesema hayo mapema hivi karibuni alipokutana na Viongozi wa Vijana Wakatoliki katika ukumbi wa Halmashauri ya Walei Jimbo, wakati wa mkutano mkuu wa idara […]

  Mwili wa aliekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la MBEYA Mhashamu EVARISTO CHENGULA, ambaye amefariki dunia jana, utaagwa siku ya Juma tatu Novemba 26 hapa jijini DAR ES SALAAM, kabla ya kusafirishwa kuelekea Jimboni Katoliki MBEYA kwa Maziko. Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kwa Vyombo vya Habari na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu […]

TANZIA Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (tec) Askofu Grevas Nyaisonga anatangaza kifo cho cha Askofu wa Jimbo katoliki la mbeya mhashamu evaristo chengula. Kilichotokea Tarehe 21/11/2018 majira ya mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa anapatiwa matibabu. Askofu Chengula alizaliwa Januari Mosi mwaka 1941 Kijijini Mdabulo na alipata Daraja […]

Na Izack B Mwacha DSM: Wito umetolewa kwa Mapadre, kuwa na utayari wa kwenda kila kona ya dunia kuihubiri injili kama ilivyokuwa kwa wamisionari wa kwanza, waliojisadaka maisha yao bila ya hofu yeyete pamoja na kwamba walijua fika hatari pamoja na vitisho vya ajabu sehemu walizokuwa wakienda. Wito huo umetolewa na Askofu msaidizi wa jimbo […]


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE