Askofu Urasa: Kanisa liwekeze kwa vijana

Written by on November 22, 2018

 

Askofu wa Jimbo Katoliki SUMBAWANGA Mhashamu BEATUSI URASA amewataka Vijana kuishi misingi ya Kanisa Katoliki, kwa kujitoa kufanya kazi kikamilifu na uaminifu, ili kuliletea Kanisa na Taifa Maendeleo.

Askofu URASA amesema hayo mapema hivi karibuni alipokutana na Viongozi wa Vijana Wakatoliki katika ukumbi wa Halmashauri ya Walei Jimbo, wakati wa mkutano mkuu wa idara ya Vijana Jimbo Katoliki SUMBAWANGA uliohusisha Vijana zaidi ya 100 kutoka Parokia 21 za Jimbo hilo.

Akihitimisha mkutano huo, amesema kuwa ni lazima Vijana kujitambua na kujitoka katika shughuli za Kiuongozi ndani ya Kanisa, kwa kufanya maboresho ya kimtazamo na kiutendaji wenye tija, kwa kuwa kipindi hiki kanisa lazima liwekeze kwa Vijana maana ni vigumu kupata maendeleo ya kila kitu ndani ya kanisa pasipo kuhusisha au kushirikisha Vijana kwa mawazo, fikra, nguvu na utendaji wao.

Aidha Askofu URASA amewataka Wazazi, Walezi na Walimu wa dini kuwasaidia Vijana waishuhudie Imani kwa kulea dhamiri zao, nia zao na kuheshimu taratibu za Kanisa na za Kijamii kwa kumjua Mungu, kwani changamoto nyingi na hatarishi Vijana vinahitaji malezi na dira ya njia sahihi toka kwa Wazazi.


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE