Askofu Ngalalekumtwa: Bikira Maria ni Kiumbe safi, teule na Jirani wa Yesu

Written by on September 26, 2018

 

Na Izack Mwacha: Iringa

Askofu wa Jimbo katoliki la Iringa Mhasham Tarcisius Ngalalekumtwa Amewataka waamini kutambua ya kuwa, hakuna mtu mwenye uwezo wa kusema au kuelezea sifa zinazomuhusu Mama Bikira Maria kwa ukamilifu wake, kwani Mama huyo ni kiumbe safi, teule na jirani wa Yesu.

 

Askofu Ngalalekumtwa Ameyasema hayo mwishoni mwa juma wakati akizungumza na Radio Maria Tanzania, Kuelekea Uzinduzi wa Kampeni ya Kapu la Mama Bikira Maria, ambayo inafanywa na Radio hiyo kwa ajili ya kuchangia Gharama za Uendeshaji, Pamoja na Ununuzi wa Magari ya Kuharakisha mawasiliano ya kuwafikia watu wengi Zaidi.

Katika mazungumzo yake na Radio Maria Tanzania Askofu Ngalalekumtwa Alieleza kuwa, Ibada na Katekesi kwa Mama Bikira Maria ni jambo la msingi kwa kila Mwanadamu mwenye Imani  kwa sababu ya Ukaribu wa Mama Bikira maria na mkombozi wa ulimwengu, nua kusema kuwa  Kupitia Mama Bikira Maria siku zote imekuwa njia sahihi ya maombi ya kila mwanadamu kujibiwa haraka Zaidi.

Akizungumzia Njia rahisi ya kutoa katekesi pamoja na mafundisho juu ya Mama Bikira Maria Askofu Ngalalekumtwa amesema kuwa Radio Maria Imekuwa moja kati ya njia sahihi ya kutoa mafundisho yenye tija juu ya Mama Bikira Maria, na hivyo kuna sababu ya kuonyesha ushirikiano mkubwa katika kuiwezesha radio hiyo ili iweze kuwa na mwanya mpana Zaidi katika kuifikisha katekesi hiyo kwwa watu wengi Zaidi.

Katika hatua nyingine Askofu Ngalalekumtwa alisema kuwa kila Mwanadamu yafaa sana awe na ukarimu, lakini ukarimu unaohusisha maswala ya kiroho ni sawa na kujiwekea ulinzi kwa Mungu naye siku zote atakulinda.

Alihitimisha kwa Kusema Kuwa Kapu la Mama ni kipindi kifupi sana ambacho watu wote wenye Mapenzi mema wanaalikwa kuichangia Radio Maria Tazania kwa lengo la kushiriki umisionari Hivyo ni kipindi cha Baraka ambacho kila mwenye tamaa ya kuwa mmisionari wa kweli Atashiriki.

Kampeni ya kapu la mama Kampeni ya pili ikitanguliwa na Mariathoni ambayo ilifanyika mwezi wa tano ambao kikanisa ni mwezi wa Mama Bikira Maria, na kampeni hii inafanyika Mwezi wa Rozari takatifu ambao pia wakristo wote wanaalikwa kusali pamoja na Radio Maria.

Uzinduzi rasmi wa Kampeni hiyo ni Ijumaa ya Tarehe 28/09/2018 ambayo itadumu mpaka tarehe 12/11/2018.

Mwisho


Current track

Title

Artist

CLOSE
CLOSE